MADRID BILA YA RONALDO NA BALE WAIFUNGA ESPANYOL NA KUFIKIA REKODI YA BARCA



1Real Madrid wameifunga Espanyol na kufikia rekodi ya Barca ya kushinda mechi 16 mfululizo kwenye ligi ya La Liga na kufanikiwa kukaa kileleni kwa tofauti ya pointi tatu na mshindi wa pili.
Magoli kutoka kwa James Rodriguez na Karim Benzema yaliwahakikishia ushindi Real Madrid na kuifikia rekodi hiyo ya Barca iliyowekwa na Pep Guardiola msimu wa 2010-11.
Real, bila ya Gareth Bale na Cristiano Ronaldo wakiwa katika dimba la Cornella-El Prat wameshinda mchezo wao wa nne ndani ya mechi nne tangu msimu mpya wa La Liga uanze.
Barcelona wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi tisa.
James Rodriguez alifunga goli baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Toni Kroos huku Benzema akifunga goli mnamo dakika ya 70 kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Lucas Vazquez.
1

Source: Shaffih DaudaRead More 
MADRID BILA YA RONALDO NA BALE WAIFUNGA ESPANYOL NA KUFIKIA REKODI YA BARCA MADRID BILA YA RONALDO NA BALE WAIFUNGA ESPANYOL NA KUFIKIA REKODI YA BARCA Reviewed by WANGOFIRA on 19:38:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.