Aliyeng’atwa ulimi Wakati Akipigana Denda na Mwanamke Ahofia Kuachwa na Mchumba Wake

Kijana Saidi Mnyambi (26) anayedaiwa kung’atwa 1/3 ya ulimi wake wakati wakinyonyana ulimi na mwanamke mmoja, ameingiwa na hofu kuwa mchumba wake anaweza kumwacha kutokana na kitendo hicho.

Kijana huyo mkazi wa Unyankhae, Manispaa ya Singida, aliyasema hayo juzi hospitalini alikolazwa .

Alisema hofu aliyonayo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na tukio hilo kuwa gumzo kubwa ndani na nje ya Singida. 

“Kabla ya tukio hilo, uchumba wangu ulikuwa unaendelea vizuri na mambo yalikuwa yanaelekea kwenye kufunga ndoa lakini sasa nina hofu mwenzangu anaweza akapotoshwa na mambo yakaharibika. Nikitoka hospitalini nitalifuatilia jambo hili kwa ukaribu zaidi ili kuweka mambo sawa,” alisema Mnyambi. 

Kuhusu matibabu, Mnyambi alisema anaendelea vizuri na kwamba sasa anaongea vizuri kama binadamu wengine na maumivu yamepungua. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Peter Kakamba alisema wanamshikilia mwanamke huyo (jina hajalitaja) aliyemng’ata ulimi Saidi na wanaendelea na upelelezi kabla sheria hazijachukua mkondo. 

Alisema mkuu wa upelelezi makosa ya jinai Mkoa wa Singida anakamilisha uchunguzi lakini akabainisha kuwa taarifa zilizoenea awali kuhusu tukio hilo ni tofauti na hali halisi. 

“Baada ya kumpata mwanamke anayetuhumiwa kumng’ata ulimi Mnyambi, zimepatikana taarifa mpya. Waandishi kuweni na subira tutawapatia taarifa zenye mashiko wakati wowote kuanzia sasa,” alisema Kakamba.
Aliyeng’atwa ulimi Wakati Akipigana Denda na Mwanamke Ahofia Kuachwa na Mchumba Wake Aliyeng’atwa ulimi Wakati Akipigana Denda na Mwanamke Ahofia Kuachwa na Mchumba Wake Reviewed by Unknown on 21:10:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.