Usimamizi bora wa biashara kwa wale ambao bado wameajiriwa.




Kutokana na kipato cha mshahara wa kwenye ajira kutokutosheleza mahitaji, waajiriwa wengi wamekuwa wakianzisha biashara zao za pembeni. Hii pia imekuwa ni njia ya kujiandaa kutoka kwenye ajira na kwenda kujiajiri wao wenyewe ili kuwa na uhuru mkubwa wa maisha yao. Ni kitu kizuri sana kwa waajiriwa kuweza kuendesha biashara huku bado wameajiriwa.Watu wengi ambao wanaendesha biashara wakiwa bado wameajiriwa huwa wanakutana na changamoto kubwa sana kwenye usimamizi wa biashara zao. Hii hupelekea biashara hizo kushindwa kukua na kupelekea kufa kabisa kwa biashara hizo. Hili limekuwa linawaumiza watu wengi na kuwakatisha tamaa, wengine wasithubutu tena kuingia kwenye biashara.
KUPATA KITABU HIKI BONYEZA MAANDISHI HAYA.
Leo kupitia makala hii ya KONA YA MJASIRIAMALI, tutakwenda kujifunza namna bora ya kusimamia biashara yako kama bado umeajiriwa, ili uweze kukuza biashara hiyo na baadaye kuweza kuondoka kwenye ajira na kusimamia biashara yako moja kwa moja ili kuwa na uhuru kwenye maisha yako.Wafanyabiashara wengi ambao bado ni waajiriwa wana changamoto moja kubwa sana ambayo ni muda. Wengi wamekuwa wakibanwa muda kwenye ajira zao na hivyo kukosa muda wa kuzifuatilia biashara zao kwa karibu. Pia watu hawa wamekuwa na changamoto ya nguvu, wengi wanatoka kwenye kazi zao wakiwa wamechoka sana na hivyo kushindwa kufanya mambo makubwa kwenye biashara zao. Hizi ni changamoto ambazo kila mfanyabiashara ambaye bado yupo kwenye ajira anahitaji kuzifanyia kazi ili aweze kuisimamia biashara yake vizuri.SOMA; USHAURI; Jinsi Ya Kujua Biashara Inayolipa Eneo Ulipo.Wafanyabiashara wengi ambao bado ni waajiriwa, wamekuwa wakiwaajiri watu wa kuwasaidia kuendesha biashara zao, lakini kutokana na kukosa muda wa kufuatilia biashara hizo kwa karibu, wanawaachia watu hao kila kitu kwenye biashara. Watu hawa wanafanya kila maamuzi ya biashara kama wanavyotaka wao wenyewe. Katika maamuzi haya yapo ambayo ni mazuri na mengi ambayo siyo mazuri kwenye biashara yako. Wakati mwingine uhuru wa aina hii umekuwa unawashawishi wasaidizi wengi kwenye biashara kufanya matumizi mabaya ya rasilimali za biashara na hata kuiba na kuondoka kwenye biashara hiyo. Hali kama hizi zimekuwa zinapelekea biashara nyingi kushindwa kukua na hata kufa kabisa.Kitu kimoja muhimu sana ambacho kila mtu aliyepo kwenye biashara anapaswa kukijua ni kwamba kama unamiliki biashara, basi utajitajika kufanya mambo mengi wewe mwenyewe, kama unataka biashara hiyo ifanikiwe. Kuna vitu vingi ambavyo hakuna yeyote anayeweza kukufanyia kwenye biashara yako, bali wewe mwenyewe. Kuendesha biashara siyo kuwapangia watu majukumu na wewe kupumzika au kuwasimamia, badala yake ni wewe kufanya na wale wanaokusaidia huku ukiwaonesha ni namna gani ya kufanya, mara zote.SOMA; Njia tano (5) za uhakika za kuweza kuikuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.Wafanyabiashara ambao bado wameajiriwa wamekuwa wakilikwepa hili, wanatafuta watu wa kuwaajiri na kisha wanawaachia biashara zao. Kutokana na kukosa muda wanakuwa mbali na biashara zao wanakuja kustuka pale wanapoona biashara inakufa badala ya kukua.Lakini changamoto ni nguvu na muda, je tunawezaje kupambana na changamoto hizi ili tuweze kusimamia biashara zetu kwa ukaribu?Kwanza kabisa pangilia muda wako vizuri. Muda ulionao unatosha sana kama utaupangilia vizuri, unaweza usiwe na muda mwingi lakini huwezi kukosa walau masaa mawili au hata moja la kupita kwenye biashara yako kila siku ili kuweza kujua inaendeleaje na kujionea kwa macho yako mwenyewe. Ni muhimu uwe kwenye eneo la biashara kabisa, ili ujionee kila kinachoendelea, usikubali taarifa unazopewa kwa njia ya simu, nyingi siyo taarifa sahihi. Siku ambazo huendi kazini, kama mwisho wa wiki au siku za sikukuu, kaa kwenye biashara yako muda wote. Hata kama biashara ni ndogo, kuwepo pale na ona jinsi ambavyo wasaidizi wako wanaendesha biashara hiyo, ona jinsi wateja wanavyohudumiwa, ona jinsi maamuzi yanavyofanywa na kama huridhishwi na baadhi ya mambo toa maelekezo kipi cha kufanywa.Pia unaweza kutumia njia za kisasa za kusimamia biashara yako ambapo unaweza kufuatilia kwa karibu popote ulipo. Zipo programu za kuweka kwenye biashara yako na wasaidizi wako wakawa wanaweka taarifa za biashara na wewe kuweza kuziona popote pale ulipo. Japokuwa programu za aina hii haziondoi umuhimu wa wewe kuwepo kwenye biashara, bado unahitaji kupata muda wa kuwa kwenye biashara yako.SOMA; Sababu Tano Kwa Nini Biashara Nyingi Zinazoendeshwa Na Waajiriwa Huwa Zinakufa.Iweke biashara yako karibu na kazini kwako au nyumbani kwako. Kama biashara ipo mbali na kazini na nyumbani, utashindwa kuifuatilia kwa ukaribu, kwa sababu unapokuwa umechoka ni vigumu kwenda mbali kuangalia biashara. Lakini biashara inapokuwa karibu na kazini kwako ni rahisi kupitia pale unapotoka kazini. Na kama ipo karibu na nyumbani ni rahisi kupitia pale unapoelekea nyumbani.Muhimu zaidi ni kujitoa hasa siku za mwanzo za biashara yako, ni lazima uweze kwenda hatua ya ziada, ni muhimu ujitume hata kama umechoka. Jua ya kwamba unatengeneza uhuru wa maisha yako na weka juhudi kubwa ili kupata uhuru huo. Nakutakia kila la kheri katika ukuaji wa biashara yako.TUPO PAMOJA,KOCHA MAKIRITA AMANI.www.kisimachamaarifa.co.tz/makiritaKwa ushauri na Coachingbonyeza maandishi hayakupata utaratibu.Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembeleaMOBILE UNIVERSITY(bonyeza hayo maandishi.)

Source: Hisia za MwananchiRead More 

FacebookTwitterGoogle+WhatsAppRedditTumblr

Usimamizi bora wa biashara kwa wale ambao bado wameajiriwa. Usimamizi bora wa biashara kwa wale ambao bado wameajiriwa. Reviewed by WANGOFIRA on 21:17:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.