Mfahamu kinda mpya wa Taifa Stars anayekipiga Italia


  
Kwa mara ya kwanza , Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Charles Mkwasa ameamua kumjumuisha katikakikosi chake kitakachoivaa Nigeria , Kiungo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 19 , Said Mhando anayechezea timu ya Brescia Calcio inayoshiriki ligi daraja la pili nchini humo maarufu kama‘Serie B’ .

Mhando ni Mtanzania aliyezaliwa nchini Italia huku Baba yake akiwa ni Mtanzania na mama yake akiwa na asili ya Somalia.

Said-Mhando-Brescia-Taifa-Stars bongosoka

Mhando alianza kucheza soka akiwa na umri wa miaka mitano katika akademia yaBrescia ambapo aliweza kupandishwa ngazi moja hadi nyingine hadi katikati ya msimu ulioisha alipopandishwa rasmi kikosi cha wakubwa huku msimu huu akiwa ni mchezaji rasmi wa kikosi hicho akikabidhiwa jezi namba 16 .

Mhando anaweza kuwakilisha Tanzania kimataifa kutokana na umahiri wake wa kusakata kabumbu na pia kama msimu huu klabu yake itafanikiwa kurudi Ligi Kuu Italia kwa mara ya kwanza tangu iliposhuka msimu wa 2010-11. Pia wanasoka maarufu kama Roberto Baggio ,Pep Guardiola ,Andrea Pirlo naLuca Toni waliwahi kuichezea timu hiyo .





Source: Bongo SokaRead More
Mfahamu kinda mpya wa Taifa Stars anayekipiga Italia Mfahamu kinda mpya wa Taifa Stars anayekipiga Italia Reviewed by WANGOFIRA on 21:09:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.