Kauli ya serikali kuhusu kuhamishwa kwa stendi ya mabasi Ubungo Jijini Dar es Salaam

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewapiga marufuku mawakala wanaotoza faini za kuegesha magari vibaya katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Ubungo hadi hapo yatakapotengenezwa maeneo rasmi kwa ajili ya maegesho ya magari.

Makonda alitoa kauli hiyo jana wakati alipofanya ziara kujionea hali halisi ya kituo hicho.

Alisema haiwezekani mawakala wakaendelea kutoza faini za maegesho ambayo si sahihi wakati katika eneo hilo hakuna maeneo maalumu kwa ajili ya maegesho ya magari.

“Nataka maeneo rasmi yakishatengwa ndipo muanze kutoza faini, mmekuwa mkiwasumbua wananchi hawajui wapi ni sehemu ya maegesho na wapi si sehemu ya maegesho wekeni alama ndipo muanze kuwatoza,” alisema Makonda.

Licha ya kutoa kauli hiyo, Makonda pia alimtaka Mkurugenzi wa Jiji kabla ya kumalizika wiki hii kuhakikisha kituo hicho kinawekwa taa ili kuondoa usumbufu wanaokutana nao abiria na wananchi hasa wakati za usiku.

"Lakini kabla ya wiki hii haijaisha nataka kuona taa zote za ubungo zinawaka, sitaki kuviona vifusi katika eneo hili la stendi na baada ya siku 20 nitarejea kujionea utekelezaji wake kama umekamilika"  Alisema Makonda

Katika hatua nyingine, Makonda alisema kuwa serikali ipo katika mpango mwisho wa kuihamishia stendi hiyo kutoka ubungo kwenda Mbezi mwisho.

"Shahuku yangu ni kuwa na stendi tofauti na tuliyonayo, nataka Dar es salaam iwe na stendi ya kimataifa na tayari tunalo eneo kule mbezi ambapo halmashauri ya jiji tayari ipo kwenye mchakato wa kukamilisha ujenzi huo.

"Nataka kuihamisha hii stendi ya ubungo ili tuepukane na kero ya kukutana na mabasi ya mwendo kasi kwakuwa nayo ni moja ya changamoto, duniani kote maroli  yakiingia katikati ya mji hutumika kubeba mikate ajabu Dar es salaam maroli yanabeba ngano na makontena"
Kauli ya serikali kuhusu kuhamishwa kwa stendi ya mabasi Ubungo Jijini Dar es Salaam Kauli ya serikali kuhusu kuhamishwa kwa stendi ya mabasi Ubungo Jijini Dar es Salaam Reviewed by WANGOFIRA on 08:11:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.