Jitihada Za Kumfanya Rais Museveni Awe Rais Wa Milele Zinafanyika

NRM,Rais Yoweri Museveni-Uganda
Maofisa wa chama cha National Resistance Movement (NRM) kinachotawala nchini Uganda wamepitisha uamuzi wa kupeleka bungeni mapendekezo ya kuondoa kikwazo cha umri katika katiba ya nchi hiyo kinachomzuia Rais Yoweri Museveni kugombea tena katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo unaotarajiwa kufanyika 2021.
Rais Yoweri Museveni ambaye alizaliwa tarehe 15 Agosti mwaka 1944 anafikisha umri wa miaka 72 mwaka huu. Kwa mujibu ya katiba ya sasa ya Uganda mtu mwenye umri unaozidi miaka 75 haruhusiwi kugombea Uraisi nchini humo. Kwa maana hiyo Rais Museveni ataruhusiwa kugombea endapo tu kipengele hicho kitabadilishwa.
Kwa mujibu wa Associated Press, Rais Museveni ambaye alichukua madaraka kimabavu mwaka 1986 anamaliza msimu wake wa uongozi mwaka 2021. Atakuwa amefikisha umri wa miaka 77.
Msemaji wa Rais Museveni, Don Wanyama, amenukuliwa akisema kabla ya mkutano mkuu baadhi ya maofisa wa chama tawala walikuwa wameanzisha petition ili kuondoa kipengele hicho cha umri. Kwa sababu chama cha NRM kina wabunge wengi bungeni, hoja hiyo inaonekana kuwa na kila dalili za kupita.
Mwaka 2005 kipengele cha ukomo wa urais kwa mihula miwili ili kumruhusu Rais Museveni kugombea tena wakidai kwamba bado anapendwa. Tangu hapo ameshashinda uchaguzi mkuu mara tatu ingawa kila mara wapinzani wamekuwa wakilalamika kwamba chaguzi zimekuwa sio za haki.

Source: Bongo CelebrityRead More 
Jitihada Za Kumfanya Rais Museveni Awe Rais Wa Milele Zinafanyika Jitihada Za Kumfanya Rais Museveni Awe Rais Wa Milele Zinafanyika Reviewed by WANGOFIRA on 20:32:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.