BALOZI WA CHINA, MAKONDA, WASHUSHA NEEMA NDONDO CUP

IMG_0520
Usiku wa August 4 ubalozi wa China nchini Tanzania chini ya balozi Dkt. Lu Youqing ulizialika timu tatu zilizofanya vizuri kwenye mashindano ya Sports Extra Ndondo Cup msimu huu wa 2016.
Timu zilizoalikwa kwenye chakula cha jioni kwenye ubalozi wa Chini ni pamoja na washindi wa tatu wa mashindano hayo Makumba FC, washindi wa pili Kauzu FC na mabingwa wa michuano hiyo Temeke Market.
Timu hizo ziliongonzwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda, uwakilishi kutoka shirikisho la soka Tanzania (TFF) na uwakilishi kutoka chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRAFA).
Balozi wa China nchini Tanzania amesema, amevutiwa na mapenzi ya soka waliyonayo watanzania hasa kuanzia katika ngazi ya chini licha ya wachezaji kucheza kwenye viwanja vyenye ubora duni lakini bado wanapambana kutimiza ndoto zao.

IMG_0520IMG_0502
“Mchezo wa soka ndiyo unapendwa zaidi Tanzania, katika fainali ya Ndondo Cup nimeshuhudia upendo wenu kwenye soka ingawa uwanja wa michezo si mzuri sana lakini haiathiri shauku yenu,” amesema balozi huyo ambaye alihudhuria mchezo wa fainali ya Ndondo Cup kati ya Kauzu FC dhidi ya Temeke Market uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari.
“Nimekubaliana na Mh. Makonda kwamba atatupa mpango wa kuboresha uwanja wa michezo mkoani Dar es Salaam na kama ubalozi wa China tutawasaidia vijana wetu kadiri tuwezavyo kuboresha hali ya michezo.”
“Mchezo wa soka unaendelea kwa kasi sana nchini China. Ligi kuu ya China ni miongoni mwa ligi hodari duniani, klabu ya Guangzhou Evergrande ilishinda klabu bingwa ya soka barani Asia.”
“Wachezaji wengi kutoka nchi tofauti wanajiunga na ligi ya China miongoni mwao wengi ni kutoka Afrika. Ni matumaini yetu kwamba siku za mbele wachezaji wa Tanzania wataweza kujiunga na ligi hiyo.”
IMG_0502
“Vijana ndiyo kipaumbele cha taifa. Naamini ninyi nyote mtaendelea kudumisha amani na mshikamano na kukaa mbali na vurugu, kutumia wakati vizuri kujifunza kwa bidii na kujishughulisha na kazi za za ujenzi wa taifa.”
“China ni rafiki mzuri wa Tanzania, serikali na watu wa China wataendelea kuungana nanyi na kutoa michango mikubwa kwa ujenzi wa taifa la Tanzania na wa urafiki kati ya China na Tanzania.”
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda amesema, bado nia yake ya kuwasaidia vijana wa hali ya chini wenye vipaji katika michezo iko palepale. Makonda ameonza kwamba, lengo lake ni kuhakikisha wachezaji ambao hawana uwezo wa kucheza kwenye uwanja wa taifa na viwanja vingine vyenye ubora wanapata fursa ya kuonesha vipaji vyao wakiwa katika viwanja angalau vyenye ubora unaoridhisha ndiyo maana anapambana kukarabati viwanja ili vijana wacheze.

IMG_0504IMG_0504
“Wakati natoa ahadi ya kuboresha viwanja vitatu kila mwaka kwenye mkoa wa Dar es Salaam sikua najua pesa itatoka wapi, lakini kwasababu nipo karibu na nina mahusiano mazuri na wadau wakubwa wa mchezo wa soka, nilijua hili jambo lazima litafanyika.”
Balozi wa China nchini Tanzania kwa niaba ya serikali ya watu wa China ameahidi kukarabati viwanja vitatu mkoa wa Dar es Salaam. Lakini pia Mh. Paul Makonda amemkabidhi ramani ya baadhi ya viwanja vinavyotakiwa kuwa.
IMG_0509

Source: Shaffih DaudaRead More 
BALOZI WA CHINA, MAKONDA, WASHUSHA NEEMA NDONDO CUP  BALOZI WA CHINA, MAKONDA, WASHUSHA NEEMA NDONDO CUP Reviewed by WANGOFIRA on 20:26:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.