WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUWA CHACHU YA MABADILIKO YA UKUAJI WA UCHUMI NCHINI
Katibu
Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu wa mkoa wa Dodoma Bw.
Deogratius Nyinza (kulia) akifunga kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii vilivyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto mjini Dodoma.Katikati ni Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimali watu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Bw.Erasimus Rugarabamu na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii
Bw.Enterberth Nyoni (kushoto).
Wakuu
wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyo vilivyo chini ya Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia kwa makini
hotuba ya ufungaji wa mkutano huo iliyokuwa ikitolewa na Katibu Tawala
Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu wa mkoa wa Dodoma Bw. Deogratius
Nyinza mjini Dodoma.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli anayeshughulikia Taaluma
Bi. Columba Maboko akizungumza kwa niaba ya Washiriki wenzake
waliohudhuria kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati
kufunga kikao hicho mjini Dodoma.
Wakuu
wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakiwa katika picha ya pamoja na
Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu wa mkoa wa Dodoma Bw.
Deogratius Nyinza (katikati mstari kwanza) na baadhi ya viongozi wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Na.Aron Msigwa - DODOMA.
Watumishi
wa Umma wametakiwa kufanya kazi kwa bidii, weledi na maarifa na kuwa
tayari kukubali mabadiliko yanayotokea ndani ya Utumishi wa Umma ili
kuliwezesha Taifa kufikia malengo yaliyokusudiwa katika utoaji wa huduma
bora kwa wananchi.
Kauli
hiyo imetolewa mjini Dodoma na Katibu Tawala Msaidizi Utawala na
Rasilimali Watu wa mkoa wa Dodoma Bw. Deogratius Nyinza wakati akifunga
kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyo chini ya
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mjini
Dodoma.
Akizungumza
na Wakuu hao amesema kuwa wakati umefika kwa watumishi wote wa umma
kutimiza kikamilifu wajibu na majukumu yao ya kila siku katika maeneo
yao ya kazi kwa weledi mkubwa ili utendaji wao uweze kupimwa kwa kuwa na
matokeo makubwa kwa wananchi
Bw.
Nyinza amesema kuwa wao kama viongozi wa Taasisi muhimu za Elimu hapa
nchini wanapaswa kuwa chachu ya kuleta mabadiliko nchini kwa kuwa mfano
katika kusimamia rasilimali fedha katika mapato na matumizi ili wananchi
waweze kupata huduma endelevu zilizokusudiwa.
"
Najua mna sehemu kubwa sana katika kusimamia rasilimali hakikisheni
mnasimamia vizuri fedha zinazopatikana ili zilete matokeo yaliyokusudiwa
ili kuepuka mtego wa kuingia kwenye matumizi mabaya ya fedha za
umma,kagueni matumizi yote ili kujiridhisha na mambo yanayotendeka
katika maeneo yenu " Amesisitiza Bw.Nyinza.
Amewataka
wawe tayari kuzuia aina yoyote ya ufujaji wa fedha katika vyuo
wanavyovisimamia kwa kuzingatia kanuni na taratibu zinazosimamia
matumizi ya fedha huku akisisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano
inasimamia matumizi bora ya rasilimali za umma na kupiga vita matumizi
mabaya ya fedha.
Ametoa
wito kwa wakuu hao kuwa tayari kukubali mabadiliko ya mfumo wa elimu
yanayotokea nchini kwa kuweka mikakati itakayowafanya waendane na
mabadiliko yanayotokea ikiwemo uboreshaji wa Taasisi za elimu
wanazozisimamia, kujiendeleza kielimu na kubuni vyanzo vipya vya mapato
kwa lengo la kuongeza mapato ya taasisi zao.
Bw.Nyinza
amewataka Wakuu hao wa vyuo kutekeleza maazimio yaliyotokana na kikao
kazi chao ili Taifa liendelee kunufaika na mchango wao maendeleo ya Vyuo
vya Maendeleo ya jamii.
Awali
akizungumza kabla ya kufungwa kikao kazi hicho, Mkurugenzi wa Utawala
na Rasilimali watu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Bw.Erasimus Rugarabamu amewashukuru wakuu wa vyuo kwa ushiriki
mzuri waliouonyesha wenye lengo la kujenga taasisi imara za utoaji wa
elimu Bora ya Maendeleo ya jamii nchini.
Amesema
ushiriki wao katika kikao kazi hicho utawawezesha kutekeleza majukumu
yao katika viwango vinavyostahili na kuwawezesha kuziongoza taasisi zao
kwa weledi kwa kuzingatia Sheria, Sera, Kanuni na taratibu zinazosimamia
uendeshaji wa vyuo.
"
Kikao kazi chenu kimekuwa kizuri sana, mmekua na ushiriki hai wenye
lengo la kuwajengea uwezo na ufanisi wa kazi katika maeneo yenu,
ninaomba mtakaporudi katika maeneo yenu ya kazi myazingatie yote"
mliyojifunza kuleta maokeo chanya" Amesisitiza.
Amewataka
kuzingatia maadili katika utumishi wao kwa kuzingatia kuwa wao ni
watumishi wa umma pia kuwa tayari kukabiliana na changamoto ya
ukiukwaji wa maadili unaofanywa na baadhi ya watumishi walio chini yao
ili kujenga nidhamu kazini.
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli
anayeshughulikia Taaluma Bi. Columba Maboko akizungumza kwa niaba ya
Washiriki wenzake waliohudhuria kikao kazi hicho amesema kuwa wao kama
viongozi wa Vyuo hivyo wako tayari kuhakikisha Ubora wa Elimu katika
Vyuo vya Maendeleleo ya Jamii nchini unaimarishwa.
"Sisi
kama wasimamizi na viongozi tuliopewa dhamana ya kuongoza vyuo vya
Maendeleo ya Jamii nchini, Tuko tayari kuyafanyia kazi mafunzo yote
tuliyopewa ili vyuo vyetu viendelee kuzalisha wataalam bora wa Maendeleo
ya Jamii" Amesema Bi. Columba.
Amefafanua
kuwa katika kutekeleza Majukumu yao watahakikisha wanasimamia vyema
mapato na matumizi ya fedha za Serikali zinazoelekezwa katika vyuo hivyo
ili kuviwezesha vyuo hivyo kutoa huduma kwa jamii.
WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUWA CHACHU YA MABADILIKO YA UKUAJI WA UCHUMI NCHINI
Reviewed by WANGOFIRA
on
20:31:00
Rating:
No comments: