Wanafunzi wa Kiume Wavaa Sketi Shuleni Kupinga Adhabu ya Mwalimu Wao


Wavulana wanne katika shule moja nchini Uingereza wamefika shuleni wakiwa wamevaa sketi kwa muda wa siku mbili kulalamikia hatua ya mwalimu kuwaadhibu kwa kuvaa kaptura siku yenye joto kali zaidi nchini humo.
Wanafunzi hao wa darasa la mwaka wa tisa katika shule ya Longhill eneo la Rottingdean, Sussex Mashariki, walikuwa miongoni mwa wanafunzi 20 wavulana waliovalia kaptura za kuvaliwa wakati wa mazoezi badala ya suruali ndefu.
Baadhi walifukuzwa shuleni Jumanne na wengine kutengwa hadi siku iliyofuata. Waliokubali kuvua kaptura hizo na kuvalia suruali ndefu hawakuadhibiwa.
Lakini badala ya kuvalia sare kamili ya wakati wa masomo, kama walivyokuwa wameagizwa, wanafunzi wanne walirejea shuleni Alhamisi wakiwa wamevalia sketi.
Watatu waliambiwa wavue sketi hizo lakini wote kwa pamoja wakakataa na ndipo wakaruhusiwa kuendelea kukaa shuleni.
Mwalimu mkuu Kate Williams aliwaambia wanaweza kuvalia mavazi yoyote, mradi yawe ni sehemu ya sare iliyokubalika shuleni.
Wanafunzi wa Kiume Wavaa Sketi Shuleni Kupinga Adhabu ya Mwalimu Wao Wanafunzi wa Kiume Wavaa Sketi Shuleni Kupinga Adhabu ya Mwalimu Wao Reviewed by WANGOFIRA on 22:43:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.