Serikali Ya Uganda Kujenga Kiwanda Cha Kuchakata Mafuta Ghafi Na Kuwa Safi: MHONGO


Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema Serikali ya Uganda itajenga Kiwanda cha kuchakata mafuta ghafi na kuwa masafi (refinery)katika eneo la Kabaale katika wilaya ya Hoima nchini humo.

 Profesa Muhongo amesema hayo baada ya kutembelea eneo hilo nchini Uganda wakati wa vikao vya kujadili michakato ya ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Kabaale - Hoima nchini humo hadi katika bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Vilevile amesema kuwa Serikali ya Uganda imetoa jumla ya 40% ya hisa za (refinery) hiyo kwa Serikali 5 za Afrika Mashariki kabla ya Sudani kusini kujiunga.

Katika hisa hizo Tanzania imekaribishwa na kutengewa 8% za kununua hisa hizo zenye thamani ya US$150.4 Millioni. Aidha Prof. Muhongo ameishauri Serikali na Sekta Binafsi kushirikiana kununua hisa hizo.

Katika hatua nyingine ujumbe wa Tanzania na ule wa Uganda juu ya ujenzi wa bomba la mafuta umetembelea eneo la ziwa Albert na kujionea visima vilivyochorongwa tayari kwa uzalishaji wa mafuta ghafi (crude oil).

Ambapo inakadiriwa kuwepo kwa mapipa bilioni 6.5 ya akiba (reserve) na yanoyoweza kuchimbwa ni mapipa bilioni 2 (recoverable). 

Ujenzi wa Bomba la mafuta kutoka Kabaale Uganda hadi Tanga (The East African Crude Oil Pipeline ) utagharim dola za Marekani Bilioni 3.55 na litakuwa na urefu wa kilometa 1,443, na litakuwa na uwezo wa kusafirisha mapipa 200,000 kwa siku
Serikali Ya Uganda Kujenga Kiwanda Cha Kuchakata Mafuta Ghafi Na Kuwa Safi: MHONGO Serikali Ya Uganda Kujenga Kiwanda Cha Kuchakata Mafuta Ghafi Na Kuwa Safi: MHONGO Reviewed by WANGOFIRA on 08:18:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.