Riwaya ya Mwanafunzi Mchawi(A Wizard Student) - Sehemu ya Kumi.


MTUNZI: ENEA FAIDY
......Ghafla wanafunzi wenzake wakabaki kumshangaa Eddy, wakaanza kukonyezana kisha wote wakaanza kumtazama Eddy kwa wizi. 
 
Eddy hakujua lolote akaendelea kuoga kwa kujiachia sana.
Wanafunzi hao wambeya hawakukomea hapo Bali walitoka nje na kuwaita wenzao ambao pia wakaingia bafuni mle wakijifanya kunawa nyuso zao kumbe walizuga tu, lengo kuu ilikuwa kumtazama Eddy...


SONGA NAYO UJUE KILICHOJIRI....
. . ..EDDY aliendelea kuoga bila kujua kuna watu wanapiga chabo mle bafuni. Alijua wanafunzi wale wanamtazama kwa wema tu au labda wanautazama uzuri wake aliojaaliwa na Mwenyezi Mungu ambao daima unawachanganya mabinti na hata wanawake watu wazima ambao kuna wakati walimrubuni kwa kumpa vitu vya thamani ili awakubalie lakini bado hawakumpata kijana yule kutoka kwenye familia ya kitajiri ya Mr.Alloyce.

Eddy aliendelea kuoga kwa kujiamini mpaka alipofikisha mkono kwenye maeneo yake nyeti. Ghafla alishtuka sana kama vile amepigwa shoti ya umeme, macho yalimtoka kama MTU aliyekutana na simba USO kwa USO porini.

Eddy hakuamini alichokihisi, akaamua kuyapeleka macho yake moja kwa moja mpaka kwenye bustani yake muhimu. Akagundua kuwa sehemu zake za siri hazipo. Bado Eddy hakuamini akachukua maji kwenye kiganja chake cha mkono na kuyasafisha vizuri kwani alihisi hayaoni vizuri. Jibu likabaki moja tu Sehemu zake nyeti hazikuwepo.

"What! Mbona sielewi!" Eddy alichanganyikiwa kupita kiasi. Akachukua suruali yake na kuivaa kwa wizi ili watu wasimwone lakini alikuwa tayari amechelewa kwani alikuwa tayari ameshaonwa na watu wengi tu.

Bila hata kujiosha povu la sabuni alilokuwa amejipaka mwilini, Eddy alikimbia na kuingia bwenini. Akajibwaga kitandani kwa Jackson rafiki yake bila kujali kuwa sabuni iliyoko mwilini mwake ilichafua shuka.

"Eddy! Vipi mshkaji!" Aliuliza Jackson huku akimalizia kuvaa sare zake za shule.
" Nakufa Jack... Nakufa Mimi...."
" Unakufa? Mbona sikuelewi Eddy?" Jackson alikuwa haelewi chochote kinachoendelea kuhusu Eddy ingawa taarifa zilikuwa zimesambaa kwa wanafunzi wengi wa kiume.
" Eddy! Niambie umepatwa na nini? Unaniacha njia panda.."
" Jack... Nakufa... Siwezi kuishi... Nakufa..." Eddy alizidi kulia kama mtoto mdogo aliyenyimwa maziwa kwa muda mrefu. Akili yake haikufikiria kingine zaidi ya kujiua, asingeweza kuistahimil aibu ambayo ilimjia kwa kasi bila hata kupiga hodi.
"Jack..Dunia hadaa ulimwengu shujaa.. Jack me nakufa.. Waambie wazazi wangu..Nilipenda visivyopendeka ila sio kwa matakwa yangu naamini ni shetani tu.."
Maneno hayo yaliibua simanzi nzito kwa Jackson, machozi yalimzidi nguvu hivyo yakashuka kwa kasi machoni kwa Jackson.
"Hapana Eddy huwezi kufa, hebu niambie tatizo..!"
"Hata nikikwambia huwezi kunisaidia Jack.. Huwezi amini natamani kuwa hata nyuki wa mashineni kwa sasa!"
" una maana gani!"
"Mimi sio mwanaume tena... Unafikiri nitaificha vipi aibu hii? Bora nife.. Nikapumzike na wafu wenzangu.."
"Eddy! Sio mwanaume tena kivipi?"
"Uume wangu haupo!" Eddy aliposema hayo akashindwa kujizuia kulia kwa sauti. Hivyo akalia kwa sauti Kali iliyosikika bweni zima. Kwa bahati nzuri wanafunzi karibia wote walikuwa wameondoka ili wawahi mstarini.
Jackson alitazama SAA yake ya mkononi ilikuwa tayari SAA mbili kasoro.
" Eddy! Nitarudi sasa hivi ngoja nikakuombee ruhusa kuwa unaumwa, ila please usifanye lolote. Niahidi!" 

Eddy aliitikia kwa kichwa kuwa hatofanya lolote, Jackson akatoka huku akiwa na wasiwasi sana.Eddy aliona dunia inamwelemea na ni vigumu kukabiliana nayo. Machozi hayakuacha kumtiririka kila sekunde. Akili yake ikaanza kukumbuka mambo mengi, ndipo alipoupata ukweli kuwa Doreen ndiye aliyemfanyia ukatili ule Jana usiku.

Akili ya Eddy ikawa kama imefunguliwa kutoka kwenye kifungo kikali. Akamkumbuka Dorice wake, msichana ampendaye sana kuliko mwingine yeyote ila akakumbuka kuwa alishamsaliti na kumdhalilisha mbele za watu.

"U wapi Dorice mpenzi wangu! Dorice nisamehe ! Dorice haikuwa akili yangu! Nakupenda Dorice! Ingawa nakufa ila naomba unisamehe sana.... Doreen ni shetani! Hafai hata kidogo..!" Eddy alilia mpaka kamasi zilimtoka. Kichwa kikamgonga kutokana na kulia kwa muda mrefu.

Eddy aliinuka kitandani pale na kwenda moja kwa moja kwenye begi lake. Akachukua kijidaftari kidogo, akachana karatasi ndogo. Kisha akachukua kalamu akaanza kuandika ujumbe huku machozi yakililowanisha karatasi lile .

" Dorice mpenzi, nisamehe kwa yote yaliyotokea Nakupenda sana. Halikuwa kusudio langu mpaka sasa sielewi ilitokeaje. Mpaka kaburini, kumbuka upendo wangu, ujue kwamba Nakupenda! Nakufa mpenzi ila bado nakupenda!"

Eddy alimaliza kuandika ujumbe huo wa kusikitisha kisha akalikunja karatasi lile na kuliweka kitandani.Eddy alishusha suruali na kujiangalia tens sehemu zake za siri ili ahakikishe kama ni kweli. Ndio ilikuwa kweli kabisa wala so ndoto. Kilio cha Eddy kikaongezeka alishindwa kuvumilia akaona ni heri ajiondoe duniani mapema.

Eddy alifungua begi lake na kuchukua vidonge vingi alivyokuwa akivitumia kwa maumivu ya tumbo, akatafuta vidonge aina nyingine akavichanganya kwa pamoja. Lengo lake ilikuwa avitumie kama sumu ili aondokane na adha zinazomkàbili duniani. Akachukua maji yaliyokuwa kwenye kopo akalisogeza karibu. Akasali sala ya mwisho ili apokelewe vyema na malaika wa huko aendako.

*****
Doreen alikuwa darasani asubuhi ile. Alikuwa amekaa konani akiwa ametulia tuli huku madaftari yake mawili yakiwa yamefunuliwa kana kwamba alikuwa akiyasoma. Lakini tangu alipoyafunua madaftari Yale yalibaki hivyohivyo kwani Doreen alikuwa hayasomi ila aliyafunua kwaajili ya kuzuga tu. Mawazo yake yalikuwa yalikuwa mbali sana.

"Inabidi ulete uume wa mwanaume umpendaye, akiwa taabani na hamu ya mapenzi, pale anapotaka kufanya mapenzi nawewe ndipo uchukue uume wake! Umeelewa!" Maneno hayo yalijirudia kichwani mwa Doreen na kumfanya ashtuke kidogo.

Moyo ulimuuma sana Doreen kwa kumfanyia ukatili ule Eddy, alijiona yeye sio binadamu kabisa kwani hana roho ya ubinadamu. Huruma ilimshika sana, alimhurumia Eddy.

"Ataishije.. Daah! Najichukia sana kwa nilichokifanya.. Nampenda sana Eddy!" Aliwaza Doreen mpaka machozi yalimlengalenga machoni. Hakuwahi kumhurumia MTU yeyote duniani kama alivyomhurumia Eddy. Alijiona mkosaji sana kwa MTU asiye na hatia.

Licha ya yote hayo lakini Doreen hakuwa na jinsi. Ilibidi afanye vile ili atimize lengo lake lililomleta katika shule ya Mabango. Alikuwa tayari amefikia robo tatu ya kile alichotumwa. Ilibidi amalizie robo iliyobaki ya kusudio lake ndipo aibuke kinara katika ufalme ambao hauonekani kwa macho ya kawaida. Ushindi ulikuwa wake mpaka pale alipofikia.

Doreen aliwaza mambo mengi sana lakini wazo kuu lilibakia Kwa Eddy, alitamani kujua Eddy anaendeleaje kwa wakati ule lakini hakuwa tayari kumtembelea Eddy kwani aliona kama akuwa kero kubwa kwa kijana yule na ataibua chuki.
" masikini Eddy! Ila sina jinsi..!"

****
Dorice alikuwa amepelekwa kwenye utawala wa viumbe wa ajabu ambao hakuwahi kuwaona hata Siku moja. Sura na maumbo yao yalikuwa ya kutisha sana. Alijawa na woga sana, alitetemeka kama vile ampepigwa na baridi Kali. Hakuweza kuwatoroka kwani hata njia alikuwa haijui, hakuelewa amefikafikaje eneo lile. Alizidi kumwomba Mungu amsaidie na amwepushe na mabaya.

"Salam Malkia!" Alisalimia kiumbe yule aliyeambatana na Dorice kwa heshima na adabu.
Mwanamke mrembo mwenye dhahabu mwili mzima na mavazi ya kung' aa mwlini mwake akiwa ameketi kwenye kiti kizuri cha dhahabu alimwitikia kiumbe yule.
"Salam! Naona umefanya Nazi nzuri sana Leo!"
"Ndio malkia!"
"Vizuri sana, mtumishi wangu!"
Dorice alikuwa ametulia kimya akisubiri kitakachomtokea.
"Binadamu hawa jeuri sana...!"
Alisema malkia yule huku akiinua fimbo yake ya dhahabu na kumnyooshea Dorice.
Dorice aliogopa sana alijua kifo chake sasa kimewadia.
Malkia yule aliinyoosha fimbo ile ikatua moja kwa moja kwenye kifua cha Dorice.
Malkia yule akaituliza fimbo ile kwa muda wa dakika kama tano. Kisha akaachia kicheko kikali sana cha kutisha.. Doreen alizidi kupata hofu.............

ITAENDELEA.......

DOREEN ana siri nzito sana kuhusu maisha yake na hakuna aijuaye zaidi yake na mama yake mzazi kwa hapa duniani. Inamfanya awe katili kupita maelezo kwani akiwa na huruma hatoweza kufaanikiwa!!!! UKITAKA KUJUA SIRI HIYO ENDELEA KUFUATILIA SIMULIZI HII...
Riwaya ya Mwanafunzi Mchawi(A Wizard Student) - Sehemu ya Kumi. Riwaya ya Mwanafunzi Mchawi(A Wizard Student) - Sehemu ya Kumi. Reviewed by WANGOFIRA on 20:03:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.