RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 22 & 23

MTUNZI: ENEA FAIDY

.....MR ALLOYCE alishtuka sana baada ya kusikia kishindo kalikali nyuma yake. Aliachia chupa ya konyagi kisha akageuka haraka kutazama nini kinaendelea nyuma yake. Hakuamini kumuona mwanaye akiwa amejibwaga chini kama gunia la viazi. Alikuwa anathema kupita maelezo.

"Eddy!" Mr Aloyce aliita kwa mshangao mkubwa. Lakini Eddy hakuitikia zaidi ya kuendelea kuhema kwa nguvu.Mr Alloyce alitupa chini vidonge alivyokuwa amevishika, akamwinamia Mwanaye na kumgusa kifuani ili kusikiliza mapigo ya moyo. Aligundua kuwa mwanaye ni mzima alimsgukuru Mungu. Killed home hang a za Mr Alloyce ni kwamba pindi anarudi sebuleni pale, hakukuta mtu yeyote na wala hakusikia mtu akifungua mlango. 

"Ba...ba..!" Aliita Eddy kwa shida sana.
"Sema mwanangu...Mimi hapa" aliitikia Mr Aloyce.
"Usife. .!"
"Sifi nani kasema Mimi nakufa? Vipi lakini uko sawa?" Aliuliza mr Alloyce akiwa na hofu sana, alihofia kumpoteza mwanaye kipenzi. Eddy aliitikia kwa kichwa tu akimhakikishia baba yake kuwa yuko sawa.

Mr Alloyce aliendelea kumkagua Mwanaye kila sehemu akidhani labda ana majeraha kwani damu alizozikuta chumbani kwa Eddy zilimtisha Sana. Lakini alipomtazama mwanaye akagundua hana jeraha lolote mwilini mwake, hivyo maswali mengi yalijitokeza akilini mwake. Alijihoji maswali mengi lakini hakuwa na majibu yake.

"Baba... Mama anateseka sana!" Eddy aliongea sauti ndogo ya kujivuta sana akiwa bado amelala pale sakafuni.
"Anateseka wapi?" Mr Alloyce alishtuka sana.
"Alikuja hapa.. Anateseka sana na yote kwa sababu yangu...!" Alisema Eddy kwa huzuni sana huku machozi yakimlengalenga machoni.
"Eddy! Upo sawa kweli?" Mr Alloyce alihisi Eddy hayupo sawa hivyo anaropoka tu anachojisikia.
"Nimefanya makosa sana.. Namtesa mama yangu..."
"Eddy usiseme hivyo.. Unamtesa na nini?"
"Alivyotaka kunipeleka kwa mganga wameamua kumuadhibu...!"
"Kina nani?"
"Wachawi...!"
"Oh My God.." 

Maneno Yale yalizidi kumchanganya Mr Alloyce, alishundwa afanyaje kwani ilikuwa ni Mara yake ya kwanza maishani mwake kukumbana na mauzauza ya namna ile. Mara nyingi alizoea kutazama kwenye luninga tu lakini hakujua kama inaweza kumtokea kweli. Maisha yake yalikuwa machungu ndani ya muda mfupi tu kwanu matatizo aliyokuwanayo yalikuwa mazito tena yanaumiza kama gunia la misumari.
"Baba.. Nakupenda..!"
"Nakupenda pia mwanangu!"

Mr Aloyce alijikuta anashusha mchozi tu kila anapomtazama mwanaye kwanu siku zote aliamini mwanaye atakuwa mtu mkubwa sana kutokana na uwezo wake darasani. Alikuwa na akili nyingi lakini Leo amekuwa mtu wa kuteseka tu. Aliwachukia wanadamu wenzake kwa ukatili wanaoufanya juu ya familia yake.

"Baba.."
"Naam mwanangu.."
"Chukua hii." Eddy alimkabidhi baba yake kipande cha karatasi.Mr Aloyce alishtuka kidogo kisha akapokea karatasi like na kulikunjua ili alisome.Ujumbe uliokuwepo pale ulimshtua sana Mr Alloyce. Aliurudia tena"CHAGUA MOJA.
EDDY APONE TATIZO LAKE, MAMA YAKE APOTEE DAIMA. AU MAMA EDDY ARUDI, EDDY ABAKI NA TATIZO LAKE"

Mr Aloyce alibaki mdomo wazi kwa mshangao, kwani ule ulikuwa mtihani mgumu kwake."Karatasi limetoka wapi?"

*****
 Mama muuza mgahawa alikuwa kama mwehu baada ya pesa zake kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Aliambatana na mfanyakazi wake ili wamfate Doreen. Waliifuata njia aliyoelekea Doreen na kumtazama huku na kule lakini licha ya kumfuatilia kwa muda mrefu hawakufanikiwa kumuona. Walifika mpaka kituo cha mabasi kumtafuta lakini pia hawakumuona.

"Luna msichana alipita hapa, mweupe amevaa sweta jeusi na sketi ya kahawia?" Aliuliza Fetty mfanyakazi wa yule mama muuza mgahawa.
"Ni mzuri sana?"
"Ndio!"
"Alipanda basi la Mbeya na limeondoka!"

Aliwajibu kijana mmoja ambaye alionekana ni kondakta wa basi.Yule mama aliangua kilio kikali palepale kwenye kituo cha mabasi bila kujali wingi wa watu. Alilia kwa sauti Kali akiwa ameweka mikono kichwani. Watu walimshangaa mama yule wakaanza kumkusanyikia.

"Hela zaangu.. Hela zaaangu... Nitalipa nini Mimi...!"
"Mama twende basi..!"
"Nataka hela zangu... Nitafanyaje hela za watu.. Hela za mkopo" 

Alilia mama yule kwa uchungu na hasira nyingi. Watu waliendelea kumshangaa pale, lakini tayari alikuwa amelizwa na binti Doreen.

Huku mama yule akiwa analilia pesa zake, Doreen alikuwa na furaha sana kwa kupata pesa zile kwani zilimsaidia katka nauli ya kutoka Iringa kwenda Mbeya.

Doreen hakuwa na ndugu yeyote jijini Mbeya ila aliamua kwenda Huko kwaajili ya kukamilisha kazi zake hasa hasa ikiwa kupata titi la msichana mrembo.

Akiwa ndani ya basi, Doreen hakuweza kuzungumza na mtu yeyote. Alitulia kimya akiwa amejiinamia. Alionekana mwenye mawazo mengi sana tena mwenye huzuni kupita kiasi. Jirani yake Doreen ambaye ni mwanamama wa makamo kiasi kama miaka 40 au 45 alimuona Doreen akiwa katika hali ile. Alimwonea huruma na kuamua kumuita.

"We binti hujambo!" Alisema mama yule lakini Doreen alibaki kimya kama vile hakusikia anavyoitwa.
"We mdada!" Aliita na kumgusa began Doreen. Doreen aliinua kichwa na kumtazama mwanamke yule.
"Shkamoo mama!" Doreen alimsalimia kwa heshima na adabu mwanamke yule.
"Marhaba.. Mie naitwa Bi Carolina.. Unaitwa nani?"
"Naitwa Doreen!"
"Asante.. Mbona una mawazo sana? Tangu umeingia kwenye gari huna raha hata kidogo.. Una tatizo gani?" Aliuliza mwanamke yule kwa upole sana.
"Nina matatizo makubwa sana mama?" Alisema Doreen kwa unyonge wa hali ya juu.
"Tatizo gani?"
"Ni hadithi ndefu sana mama angu!" Alisema Dorice safari hii machozi yalimlengalenga machoni. Maneno Yale yalivuta usikivu wa Bi Carolina. Alitamani amsikilize zaidi.

"Mama! Acha tu.. Dunia ina mateso sana..! Sina hamu!" Doreen aliachia mchozi uliokuwa ukimlengalenga machoni. Bi Carolina alimtazama kwa huruma Doreen na kumtaka aendelee kumsimulia.

"Mama! Iringa nilikuwa naishi na mjomba wangu, tumbo moja na mama yangu! Na alinichukua baada ya wazazi wangu kufariki, aliahidi atanisomesha lakini hakufanya hivyo.

Alikuwa akininyanyasa, hanipi chakula, ananifanyisha kazi ngumu wakati anajua kabisa naumwa moyo, jana kanifukuza usiku wa manane akidai namchafulia hali ya hewa nyumbani kwake, sina hadhi. Nimeteseka sana, sins hata kwa kwenda!" Alisema Doreen kwa uchungu huku akilia. Simulizi yake ilimuumiza sana Bi Carolina akatamani kumsaidia Doreen.

"Pole sana Doreen.. Kwahiyo Mbeya unaenda kwa nani?"
"Sina ndugu huko.. Naenda tu hata kutafuta vibarua..!" Aliendelea Julia Doreen akachukua leso yake na kujifuta machozi.

"Dash pole sana.. Kwangu naishi na mume wangu na binti yangu.. Naomba nikusaidie ukaishi kwangu.." Alisema yule mama kwa huruma sana.Doreen alifurahi sana kimoyomoyo has a alivoambiwa kuna binti anaishi pale.
  
*****

Sehemu ya 23
Mr Aloyce alilishikilia karatasi lile akiwa ameinamisha kichwa chake chini, mawazo yalimjaa tele kichwani mwake. Aliwaza achague lipi kati ya Yale aliyoamriwa. 

Alijiona ana mtihani mzito sana ambao alishindwa kufaulu kwa haraka. Akawaza ni heri amrudishe mkewe ili waendelee kushughulikia tatizo la mtoto wao wakiwa pamoja. 

"Namtaka mke wangu" alisema Mr Alloyce kwa sauti ya chini kisha ghafla akasikia sauti ya kicheko kikali kisha akatazama huku na kule bila kumuona mchekaji. Aliogopa kupita kiasi. Alitetemeka kama mtu aliyeshikwa na baridi Kali.

"Umechagua vyema maana ungetaka mwanao apone.. Ungepoteza kila kitu... Mkeo yupo kule Kule alikopotelea, hajafa ila tulitaka kumfundisha adabu tu kwa kulazimisha mambo." Ilisikika sauti ile iliyoambatana na mwangwi mkali.

Mr Alloyce alizidi kuogopa, akaangaza macho huku na kule lakini hakuona mtu. Woga ulimzidia sana baada ya karatasi alilokuwa ameshika mkononi kutoweka bila kujua limeenda wapi. Alitafuta pale sakafuni lakini hakuliona, akazidi kupigwa na butwaa. Maneno aliyoambiwa kuhusu mkewe yalizidi kujirudia kichwani mwake. Alihisi kama alikuwa akidanganywa tu, mkewe alishafariki na hawezi kurudi.

"Mtu alishafariki, nitakaaje nae tena? Mh! Dunia ina maajabu...!" Aliwaza Mr Alloyce."Kweli nitamwona mke wangu? Sijui niende Leo? Mh sasa hivi ni usiku sana!" Mr Aloyce aliwaza na kuwazua ubongoni mwake. Aliamua kuwa na subira, asiwe na papara. Aliamua kuisubiri kesho yake asubuhi ili aende sehemu ambayo mkewe alipotelea ili akamchukue. 

Usiku ule ulikuwa mrefu sana kwa Mr Aloyce kwani hakuwa na hata lepe la usingizi, kila dakika alikuwa akiyafikiria matukio yote yaliyomtokea kwenye familia yake akahisi ndoto tu au mchezo wa kuigiza lakini ilikuwa kweli kabisa na alishuhudia kwa macho yake.

"Eddy! Mama yako mzima, tutaenda kumfata kesho asubuhi!" Mr Aloyce aliongea.
"Baba kweli?" Eddy alishtuka kusikia vile kwani sauti iliyokuwa ikisikika ndani mle na kumpa maelekezo Mr Alloyce, Eddy hakuisikia kabisa.
"Kweli mwanangu!"Eddy aliachia tabasamu mwanana usoni kwake. Kwani hakika taarifa zile zilimfurahisha sana.
"Kesho asubuhi na mapema nitamfuata kule aliko.."


"Yuko wapi?" Kabla Mr Aloyce hajajibu swali la mwanae alishtushwa na mlio wa simu yake . simu iliita kwa sauti kutokea kwenye moja ya sofa pale sebuleni.Mr Aloyce aliinuka na kuifuata lakini alipotazama kwenye kioo alishtuka kidogo.

*****
 Gari ilitembea kwa mwendo mrefu sana mpaka ilipofika eneo la uyole jijini Mbeya. Ndipo Bi Carolina alipoamua kuchukua simu yake na kupitisha vidole vyake laini vilivyonakshiwa kwa kucha nzuri zilizopakwa ranging nyekundu. Akatafuta namba Fulani kisha akapiga.

"Mume wangu uko wapi? Tumefika hapa uyole sio muda mrefu tutaingia hapo Nanenane!" Alisema Bi Carolina .
"Kwani upo na nani?" Ilisikika sauti ya upande wa pili.
"Aah bwana .. Tupo na abiria wenzangu... Niambie uko wapi?"


"Utanikuta Hapahapa Nanenane stendi .. Nimefika kitambo nakusubiri mke wangu!" Alisema mume wa Bi Carolina kisha simu ikakatika.


Majira ya saa moja na nusu hivi, Bi Carolina na Doreen walikuwa tayari wamewasili katika kituo cha mabasi cha Nanenane jijini Mbeya. Bi Carolina alionesha kumjali sana Doreen kwa kumkaribisha Binti huyo jijini Mbeya .

"Hii ndio Mbeya Doreen... Baridi hapa ndo kwake... Karibu sana"
"Asante mama!" Aliitikia Doreen kwa sauti ya upole sana akiwa ameachia tabasamu usoni pake.


Ghafla simu ya Bi Carolina ikaita, alipotazama ilikuwa namba ya mume wake akapokea kisha akasikiliza maelekezo . Akaelewa gari ya mumewe ilipo wakaelekea pale na kuikuta gari aina ya Prado ikiwa imepaki pembezoni mwa Barbara karibu na mango la kuingilia uwanja wa maonesho ya Nanenane.


Tabasamu pana kutoka kwa mwanaume mfupi kiasi, mnene, mwenye rangi ya kunde likamkaribisha Bi Carolina. Lakini punde tabasamu hilo la mume wa Bi Carolina likayeyuka ghafla baada ya kuona mkewe ameambatana na mtu asiyemfahamu.


"Mke wangu vipi?" Aliuliza mumewe huku akimtazama Doreen.
"Kwani vipi mume wangu?"
"Huyu nani?" Aliuliza
"Mgeni wetu.."
"Ndugu yako?"
"Hapana.. Tuachane na hayo.. Tutaongea tukifika" alisema Bi Carolina.
"Shkamoo..!" Alisalimia Doreen kwa upole sana . lakini mume wa Bi Carolina hakuitikia salamu ile.
"Mke wangu.. Usiniletee uchuro.. Huyu wa wapi..!" Alifoka
"Baba Pamela mume wangu.. Mbona uko hivo? Kuna ubaya gani kuja na mgeni?"


"Hakuna tatizo kama ungenijulisha.. Kwani ni ndugu yako?"
"Sio.. Ni mtoto tu nimeamua kumsaidia ana matatizo makubwa sana!" Alijitetea Bi Carolina lakini bado mumewe hakutaka kukubaliana nae. Hakumtaka kabisa Doreen.
"Tupeleke nyumbani..." Aliomba Bi Carolina.
"Ntakubeba peke yako.. Bila huyo mgeni wako.."


"Kuwa na roho ya utu mume wangu.. Tutamwachaje huyu mtoto barabarani hapa? Si ukatili huo.
"Nimesema simtaki mgeni wako nyumbani kwangu... Jifanye una huruma utaokota mpaka majini!" Alisema mume wa Bi Carolina kisha akafunga mlango wa gari na kuondoka zake huku akimwacha mkewe na Doreen palepale.


Bi Carolina alibaki akishangaa kitendo cha mumewe siku ile. Alimtazama Doreen aligundua kuwa analia, tena Analia kwa uchungu sana.


"Usilie mwanangu tutaenda hata na daladala.." Alisema Bi Carolina kwa upole.
"Hapana mama.. Mi niache tu wewe nenda... Nisijekuharibu familia yenu bure" alisema Doreen huku akilia.
"Siwezi kukuacha hapa Doreen, usiku sasa!" Alisema Bi Carolina.


"Hapana mama nenda!" Alisisitiza Doreen lakini Bi Carolina alizidi kumbembeleza waondoke wote. Ghafla simu ya Bi Carolina ikaita, akapokea.
"Mama Pamela! Ukitaka kuja na huyo mgeni wako, usifike kwangu... Ishia hukohuko..!" 


ITAENDELEA....
RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 22 & 23 RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi - (A Wizard Student) - Sehemu ya 22 & 23 Reviewed by WANGOFIRA on 20:46:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.