Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea Mhe. Paul Kagame wa Rwanda leo Jijini Dar





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda kwa ziara rasmi ya kiserikali. Rais Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na Rais Kagame ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame. Ziara hii ni ya siku mbili.Baada ya Hapo ataelekea Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Kufanya Mazungumzo.

Baada ya hapo wataelekea katika Viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ufunguzi rasmi ya maonesho ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya Sabasaba  leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aakiwa ameambatana na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda mara baada ya kuwasili asubuhi hii katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ziara rasmi ya siku mbili ya kiserikali. Rais Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na Rais Kagame ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakipata Gwaride la heshima uwanjani
   .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakitazama kikundi cha ngoma za asili kilichokuwa kikitumbuiza uwanjani hapo.
Rais Paul Kagame akiwapungia mkono baadhi ya wananchi mbalimbali waliofika kumlaki uwanjani hapo,kushoto kwake ni  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.


 PICHA ZOTE KWA HISANI YA IKULU.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea Mhe. Paul Kagame wa Rwanda leo Jijini Dar Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea Mhe. Paul Kagame wa Rwanda leo Jijini Dar Reviewed by WANGOFIRA on 08:18:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.