ASSUMPTER MSHAMA AANZA KAZI NA WANAOKUMBATIA ARDHI
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU
mpya wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama ametoa miezi 6 kwa taasisi
mbalimbali na wananchi walio na maeneo makubwa ambayo hawayaendelezi
kuyaendeleza katika muda huo na atakaekaidi hati yake itafutwa kwa
mujibu wa sheria.
Amesema
wapo watu na taasisi mbalimbali ambazo zimekumbatia maeneo makubwa
pasipo kuyaendeleza na kuyaacha pori hali inayosababisha kuwa maficho ya
kiuhalifu..
Aidha
Assumpter amewataka watendaji wa kata,maafisa tarafa na wakurugenzi wa
halmashauri zilizopo wilayani humo kuhakikisha wanakamilisha zoezi la
upatikanaji wa madawati ifikapo July 29 mwaka huu.
Mkuu
huyo wa wilaya alitoa maagizo hayo mjini Kibaha kwenye mkutano
alioundaa ili kuzungumza masuala mbalimbali ya wilaya kwa watumishi wa
halmashauri za wilaya,wakuu wa idara ,maaafisa tarafa na watendaji wa
kata .
Assumpter
alieleza kuwa mtumishi atakayeshindwa kutekeleza maagizo hayo kwenye
sehemu yake ya kazi atakuwa amejifukuzisha kazi mwenyewe.
Alisema
hatomfumbia macho mtu ama taasisi yeyote ambayo imechukua maeneo yaliyo
umbali wa km.5 kutoka barabara kuu katika kipindi kirefu
bila kuyashughulikia.
Hata
hivyo Assumper alisema NSSF ina jumla ya eneo lenye hekta 7.5 sawa na
hekari 18 huko Mkoani B,ambalo lilichukuliwa kwa ajili ya kujenga
makazi lakini halijaendelezwa tangu mwaka 1997 lilipomilikishwa.
“Taasisi
za aina hii siwezi kuzikumbatia hata kidogo,ni lazima haki itendeke
,nina msuli nalo jambo hili.Na kuna watu wengine wanakaa katika eneo
lile kwa miaka 12 sasa ambapo wanahitajika waondolewe
“alisema Assumpter.
“alisema Assumpter.
Alisema
haiwezekanai taasisi ama mtu anahasi eneo lake kwa bila kulihudumia
halafu baada ya miaka 10/20 ndipo anajitokeza na kuondoa wananchi ambabo
wameshakaa katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 12.
Alieleza
wapo wawekezaji wengi wenye nia ya kuwekeza hivyo ni vyema kuyachukua
maeneo hayo yasiyofanyiwa kazi kwa maslahi ya mtu binafsi.
Akizungumzia
suala la madawati aliwataka watumishi hao wasilale usiku na mchana
,watafute mbinu za kufikia lengo la idadi ya madawati ambayo
yanahitajika wilayani hapo.
Assumpter alisema ni wajibu wa kila mmoja ndani ya jamii kuguswa na suala hilo la kielimu ili kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa lengo la kuondokana na uhaba wa madawati mashuleni.
Alitoa
agizo jingine la kuweka mji safi kuanzia mailmoja Kibaha hadi Mlandizi
kwani Mji wa Kibaha upo usoni mwa barabara kuu ya Morogoro.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha Lucy Kimoi,alisema wamepokea maagizo yote na watenda kuyafanyia kazi.
Akitolea
ufafanuzi juu ya suala la madawati Lucy alisema ,halmashauri hiyo
ilikuwa na upungufu wa madawati katika shule za msingi 9,162 ambapo hadi
kufikia June 30 walikuwa tayari wametengeneza na kukarabati madawati
6,979 hivyo kwasasa wana upungufu wa 2,183.
Lucy
alisema katika upande wa shule za sekondari mahitaji ya meza yalikuwa
7,032 vilivyopo ni 6,041 na kubakia na upungufu wa meza 991 huku viti
walivyokarabati na kutengeza ni viti 6,099 kukiwa na upungufu wa
viti 933 hadi sasa.
Nae
afisa ardhi halamashauri ya Mji wa Kibaha,Gilly Simiyu alisema
wataendeleza kushughulikia masuala ya migogoro ya ardhi kwa wakati kama
walivyoagizwa na mkuu huyo wa wilaya.
Alisema
kisheria huwezi kufuta matumizi ya ardhi katika maeneo yanayomilikiwa
kihalali kwa urahisi bila kufuata sheria ikiwemo kuwapa taarifa
wamiliki kisha kufuata taratibu za kufutiwa hati .
Mwisho
ASSUMPTER MSHAMA AANZA KAZI NA WANAOKUMBATIA ARDHI
Reviewed by WANGOFIRA
on
20:54:00
Rating:
No comments: