Askofu Gwajima ni Mgonjwa.....Ashindwa Kutokea Mahakamani Kwenye Kesi Inayomkabili

PETER Kibatala wakili wa Josephati Gwajima Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima jana aliiomba mahakama kuahirisha tarehe ya kusikiliza kesi inayomkabili askofu huyo sababu anaumwa.
 
Kibatala alidai mahakamani Kisutu kuwa kutotokea kwa mteja wake jana kulitokana na yeye kuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Wakili huyo  aliwasilisha madai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Syprian Mkeha Hakimu Mfawidhi anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili Gwajima

Mahakama ilikubali ombi hilo na kwamba kesi hiyo itatajwa tena 2 Agosti mwaka huu.

Katika kesi hiyo Gwajima anadaiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam.

Gwajima anadaiwa kufanya tukio hilo kati ya 16 na 25 Machi, mwaka 2015 katika Viwanja vya Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Askofu Gwajima ni Mgonjwa.....Ashindwa Kutokea Mahakamani Kwenye Kesi Inayomkabili Askofu Gwajima ni Mgonjwa.....Ashindwa Kutokea Mahakamani Kwenye Kesi Inayomkabili Reviewed by WANGOFIRA on 22:02:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.