WHO yafafanua maambukizi ya Zika hayana uhusiano na mikusanyiko.

Mkutano kuhusu virusi vya Zika.
Mkutano kuhusu virusi vya Zika.

Shirika la afya duniani linasema mikusanyiko mikubwa wakati wa kipindi cha michuano ya Olimpiki nchini Brazil haina maana kwamba washiriki wako hatarini kuambukizwa virusi vya zika.

Kamati ya dharura ya WHO juu ya ugonjwa wa ZIKA ilikutana Jumanne ili kuangalia uwezekano wa hatari katika mikusanyiko mikubwa ya watu katika miji na nchi iliyo na mlipuko wa ZIKA ikiwa ni pamoja na Rio De Janeiro.

Kamati hiyo ilieleza hatari ya mtu mmoja mmoja katika maeneo ya maambukizo iko sawa bila kujali kuna mkusanyiko au la na inaweza kupungua kwa kufuata masharti ya afya.

Idara hiyo ya umoja wa mataifa inasema kuna hatari ndogo kwamba michuano ya olimpiki ya mwezi Agost inaweza kusambaza Zika kimataifa.
WHO yafafanua maambukizi ya Zika hayana uhusiano na mikusanyiko. WHO yafafanua maambukizi ya Zika hayana uhusiano na mikusanyiko. Reviewed by WANGOFIRA on 20:38:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.