Wasiotumia Mashine za EFDs Marufuku Kufanya Biashara na Serikali



KUANZIA Julai mosi mwaka huu, serikali imepiga marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki - EFDs.
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema hayo jana bungeni wakati akiwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma jana. 
 
Aidha, Dk Mpango aliwapongeza wafanyabiashara walioitikia matakwa ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi ambayo inamtaka kila mfanyabiashara isipokuwa wale ambao wametangazwa rasmi na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato kutotumia mashine za EFD kutoa risiti kila anapouza bidhaa au huduma.
 
Alisema ili kuwa na usimamizi mzuri wa fedha za serikali na kuhakikisha kwamba zinatumika kama ilivyokusudiwa, kwa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Fedha za Umma na kanuni zake, alitangaza kuwa malipo yote lazima yaambatanishwe na ankara za madai au stakabadhi (tax invoice) zilizotolewa na mashine za EFD.
 
“Kwa sababu hiyo kuanzia tarehe 1 Julai 2016, ni marufuku kwa Wizara, Taasisi, Wakala za Serikali, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kufanya biashara na wazabuni na wafanyabiashara wengine ambao hawatumii mashine za kielektroniki - EFDs.
Wasiotumia Mashine za EFDs Marufuku Kufanya Biashara na Serikali Wasiotumia Mashine za EFDs Marufuku Kufanya Biashara na Serikali Reviewed by WANGOFIRA on 20:52:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.