Wanafunzi 24,000 kutojiunga na kidato cha 5 TZ
Kati
ya wanafunzi 393,734 waliokalia mtihani wa kidato cha nne nchini
Tanzaniamwaka uliopita,takriban wanafunzi 24,528 ambao walipita mtihani
huo huenda wasijiunge na kidato cha tano mara moja kutokana na uhaba wa
madarasa.
Kulingana
na gazeti la The Citizen nchini humo wale watakaoathiriwa ,ni pamoja na
wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na taasisi za kiufundi zilizopo
nchini humo.
Shule za uma hazitaweza kuchukua wanafunzi wote waliofuzu kuendelea na kidato cha tano.
Akitangaza
matokeo hayo ya wanafunzi waliochaguliwa ,waziri katika ofisi ya rais
anayesimamia utawala wa kijimbo na serikali za mtaa Bw George
Simbachawene alisema: ''ni swala lenye changamoto lakini tunafanya
juhudi kuhakikisha kuwa madarasa zaidi yanajengwa ili wanafunzi wote
waliofuzu waendelee na masomo''.
Kulingana
na The Citizen,amesema kuwa wanafunzi walioachwa nje ni pamoja na
wasichana 6,789 na wavulana 17,739.
Wanafunzi 24,000 kutojiunga na kidato cha 5 TZ
Reviewed by WANGOFIRA
on
23:18:00
Rating:
No comments: