UNYAMA! UNYAMA! UNYAMA! BABA AMBAKA MWANAE WA MIAKA MITATU NA KUMFANYA MKE


Mtoto mwenye umri wa miaka mitatu aliyekuwa akibakwa na baba yake mzazi na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri pamoja na kutokwa uchafu sehemu hizo ambazo ni mbegu za kiume.


Baba anayedaiwa kumbaka mtoto wake Ngassa Sekwa mkazi wa kata ya Maganzo wilayani Kishapu akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi wilayani humo



Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Hawa Ng'humbi akiwa amembeba mtoto wa miaka Mitatu ambaye alikuwa akibakwa na baba yake kila siku na kumgeuza kama mke, ambapo babayake huyo amesha achana na Mke wake tangu mwaka jana.


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng'humbi akiongea na waandishi wa habari na kukemea kitendo hicho cha kinyama huku akivitaka vyombo vya dola kutoichezea kesi hiyo bali mtuhumiwa anatakiwa afungwe jela ili liwe fundisho na kukomesha vitendo vya ubakaji ambavyo vimekithiri wilayani humo ikiwa mpaka sasa watoto 5 tayari wameshabakwa huku wanafunzi watano wakibebeshwa ujauzito.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Maganzo wilayani Kishapu wakiwa kwenye kituo cha polisi Maganzo wakishuhudia tukio hilo la kinyama.

Picha ya Mtoto mwenye nguo nyekundu kwa mbali ndiye aliyebakwa na baba yake mzazi akiingizwa ndani ya kituo cha polisi kwa ajiri ya kumstili na kumrudisha nyumbani, huku wananchi na watoto wenzie wakiwa wanasikitishwa na kitendo hicho kama unavyo waona kwenye picha.



*******


Mwanaume anayefahamika kwa jina la Ngasa Sekwa mkazi wa kata ya Maganzo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumgeuza mke mtoto wake wa miaka mitatu ambaye amekuwa akimbaka mara kwa mara na kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.


Mtuhumiwa huyo ambaye ameshaachana na mke wake 2015 ambapo mtoto wake alimpeleka kuishi kwa bibi yake, lakini alikuwa akimfuata kila siku mtoto huyo ambaye (jina limehifadhiwa) akidai anapenda kukaa na mwanaye kumbe alikuwa akimbaka kisha kumrudisha majira ya jioni kwa bibi yake mahali anapolelewa.


Akizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng’humbi Kwenye kituo cha Polisi Maganzo, bibi wa mtoto huyo Milembe Luhende alisema baba yake alikuwa akimfuata mtoto kila siku, pale anapotoka kwenye shughuli zake za ulinzi na kwenda naye kwake na kisha kumrudisha jioni ambapo siku moja alimuona mjukuu wake akiwa katika isiyokuwa ya kawaida.


“Baba ambaye amembaka mtoto wake ni mtoto wangu mimi wa kumzaa, hivyo siwezi kumsingizia na nimekasirishwa sana na unyama aliokuwa akimfanyia mjukuu wangu na nimefikia hatua ya kumshtaki ili achukuliwe hatua kali za kisheria maana huwezi kumgeuza mke mtoto wa miaka mitatu,”alisema Luhende.


"Siku ya tarehe 7/6/2016 ,mjukuu wangu alipochukuliwa na baba yake aliporudishwa nilimuona hakuwa katika hali ya kawaida pia alikuwa akijikuna sehemu za siri, na nilipoanza kumuogesha nilimuona amevimba sehemu zake za siri huku akitokwa na uchafu ambazo ni mbegu za kiume na kushtukia mchezo huo mchafu aliokuwa akifanyiwa”,aliongeza.


Bibi huyo alifafanua kuwa mara baada ya kuona hali hiyo alitoa taarifa kwa uongozi wa Kijiji na Kata na kuchukua hatua ya kwenda kushtaki pia kwenye Kituo cha Polisi ambapo walimchukua mtoto na kumpeleka kwenye kituo cha afya na kubaini mjukuu wake alikuwa amebakwa.


Kaimu mkuu wa kituo cha polisi Maganzo Osca Shani alikiri kufanyiwa uchunguzi wa kitalaamu mtoto huyo, na kubainika kubakwa ambapo pia walimuuliza maswali na kumtaja baba yake kuwa ndiye kamfanyia kitendo hicho, na kisha kumkamata mtuhumiwa na kumsweka rumande ili sheria ichukue mkondo wake.


Mkuu huyo wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng’humbi ambaye alifika kushuhudia tukio hilo, alivitaka vyombo vya dola kutoichezea kesi hiyo nakutaka Mtuhumiwa huyo afikishwe Mahakamani haraka na kufungwa jela ili kuondoa matatizo ya ubakaji wilayani humo ambapo mpaka sasa watoto 5 wameshabakwa.
UNYAMA! UNYAMA! UNYAMA! BABA AMBAKA MWANAE WA MIAKA MITATU NA KUMFANYA MKE UNYAMA! UNYAMA! UNYAMA! BABA  AMBAKA MWANAE WA MIAKA MITATU NA KUMFANYA MKE Reviewed by WANGOFIRA on 20:31:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.