Ugonjwa usiojulikana waua watu 7 na 21 kulazwa mkoani Dodoma.


Watu saba wamefariki na wengine 21 wamelazwa kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa ajabu katika wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma huku dalili zake zikiwa ni kutapika,kuharisha,kupata rangi ya manjano machoni na sehemu zingine na tumbo kuvimba na kujaa maji ambapo inaaminika watu wa kwanza kubainika kuugua walikula nyama vya ng’ombe aliyevunjika mguu katika kijiji cha Mwaikisabe wilayani Chemba.
Akizungumzia kuibuka kwa ugonjwa huo ambao umezua taharuki kwa wakazi wa mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto mhe Ummy Mwalimu amesema tayari sampuli za ugonjwa huo zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa ajili ya uchunguzi huku akiwatoa hofu wakazi wa mkoa huo ambao wanahisi huenda ukawa ni ugonjwa wa kimeta. 
Mbali na kushambulia binadamu lakini pia ugonjwa huo umezuru wanyama wafugwao wakiwemo mbwa na paka kwa upande wake Dk James Chalz Mganga Mkuu wa mkoa wa Dodoma anasema bado wataalam wa magonjwa mkoani Dodoma wanaendelea na uchunguzi huku akidai kuwa wagonjwa wanaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma pamoja na hospitali ya wilaya ya Kondoa.
Ugonjwa usiojulikana waua watu 7 na 21 kulazwa mkoani Dodoma. Ugonjwa usiojulikana waua watu 7 na 21 kulazwa mkoani Dodoma. Reviewed by Unknown on 20:56:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.