Sita Wafariki Wakibatizwa Mtoni

NB-Siyo picha katika  habari hapa chini

Watoto sita wamekufa maji bila kutarajiwa katika sherehe za kubatizwa kwao katika mto nchini Zimbabwe. Watoto watatu walinusurika kufa maji ya mto huo ambao maji yake ni ya baridi.
 
Watoto hao walionekana wakitetemeka kutokana na baridi wakati miili ya wenzao waliokufa maji ikiopolewa majini.

Polisi nchini Zimbabwe wamewatia mbaroni watu wawili ambao ni wafuasi wa dhehebu hilo la Kikristo.

Lakini pia walimjumuisha mama mmoja ambaye alidai kwamba yeye ni nabii ambaye alisema kwamba alifanya jaribio la kufufua wafu wakati wa ibada zake .
Sita Wafariki Wakibatizwa Mtoni Sita Wafariki Wakibatizwa Mtoni Reviewed by WANGOFIRA on 20:32:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.