Serikali Yamiliki Hisa Za TTCL Kwa Asilimia 100

Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano  (Mawasiliano) Dkt. Injinia Maria Sasabo akiishukuru kampuni ya Bharti Airtel kwa kuuza hisa 35 ili Serikali iweze kuendeleza mikakati yake ya kuimarisha TTCL. Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL (wa kwanza kulia) na Bwana Lawrence Mafuru, Msajili wa Hazina (wa kwanza kushoto) wakifuatilia tukio hilo.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imefanya makabidhiano ya hati ya kuiwezesha Serikali Kumiliki Hisa za Kampuni ya TTCL kwa asilimia 100 ambapo hisa ailimia 35 zilikuwa zinamilikiwa na Kampuni ya Bharti Airtel.
 
Utiaji saini huo umefanyika baina ya Bwana Larewnce Mafuru, Msajili wa Hazina na Bwana Christian Manuel De Faria, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Afrika.
 
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2016 kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kushuhudiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Dkt. Injinia Maria Sasabo, Prof. Tolly Mbwete, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL na Dkt. Kamugisha Kazaura, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
 
Kabla ya tukio hilo la leo, Serikali kupitia TTCL ilikuwa ina miliki hisa hizo kwa alisimia 65 na Bharti Airtel kwa asilimia 35.

                  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, 
                         Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Serikali Yamiliki Hisa Za TTCL Kwa Asilimia 100 Serikali Yamiliki Hisa Za TTCL Kwa Asilimia 100 Reviewed by WANGOFIRA on 20:31:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.