RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Saba

Mtunzi:  Enea Faidy


.....DOREEN alimkubalia Eddy kuwa mpenzi wake lakini alimweleza kuwa kuna sharti ambalo Eddy lazima alifuate ndipo awe nae.Dorice hakutaka kukubali kirahisi kumwachia Doreen kuwa na Eddy hivyo alipanga kulipiza ili Doreen asije kumsahau.Mwalimu John alipigwa na mkewe mpaka akapoteza fahamu ambapo mkewe alichanganyikiwa sana baada ya kumwamsha bila mafanikio....

Endelea.....
...MWALIMU JOHN alikuwa kimya pale kitini akiwa hana fahamu yoyote, mkewe akazidi kuchanganyikiwa sana kwani alihisi tayari mumewe ameaga dunia.

"Jamani mume wangu amka bado nakupenda! Nisamehe Mimi John wangu!" Alizidi kulia mke wa mwalimu John kwa huzuni na majuto makali. Alijiona mjinga sana kwa kujichukulia maamuzi mkononi bila hata kumdadisi vizuri.

Simanzi ilimtanda mwanamke yule bila kujua la kufanya, machozi yalichuruzika kama mito miwili usoni kwake kwani ndio kwanza ndoa yao ilikuwa changa kabisa tangu waoane miezi mitano iliyopita sasa iweje John aage mapema kiasi hicho? Mkewe aliufikiria upweke ambao angekabiliana nao Siku za usoni. Huzuni ikamzidia.

Mwalimu John akiwa bado ameyafumba macho yake akahisi yumo kwenye usingizi mzito sana lakini alikisikia vyema kilio cha mkewe.

Alitamani aamke ili amtulize mkewe lakini mwili ulikuwa kama umegandishwa na sumaku. Hakuweza hata kutikisika, ghafla akahisi upepo mkali sana ndani ya nyumba yake alipotazama ukutani akakutana na sura ya kutisha sana.

Huku ikifuka moshi mdomoni, macho mekundu kama damu na kichwani yalichomoza mapembe mawili marefu. John aliogogopa sana kwani tangu azaliwe hakuwahi kukutana na kiumbe wa ajabu na wakutisha namna ile. Alitamani azinduke usingizini lakini hakuweza, hivyo alibaki akitetemeka.

Ghafla kiumbe yule akabadilika na kuwa sura ya msichana mrembo sana. Mwalimu John akabaki kinywa wazi akistaajabu ya Mussa. Alipotazama vizuri aligundua ni Doreen , akashtuka sana.Doreen alimtazama mwalimu John kwa dharau sana kisha akaachia kicheko kikali sana.

"Mimi ni Doreen Mbwana! Daima usinichezee maana sichezewi kirahisi.. Unataka kuniendea Malawi we? Hahahahah umechelewa sana John, nina nguvu kuliko unavofikiria"

Doreen akamsogelea John, na kutoa kucha zake ndefu nyembamba kama msumari kisha akamgusa mdomo John."Umeniita Nimekuja! Sasa utaipata fresh...! Hahahahahahahhh" alisema Doreen kisha akatoweka . John alihema kwa nguvu sana huku woga ukiwa umemtawala kupita kiasi kwani maneno ya Doreen yalimtisha.

Mke wa Mwalimu John alizidi kulia baada ya kuona mumewe haamki kwa muda mrefu. Kelele Za kilio chake ziliwafikia majirani ambao walikuja kwa wingi kushuhudia kilichotokea. Bila hodi majirani hao walitiririka kama utitiri nyumbani kwa mwalimu John.
"Kuna nini jirani?" Aliuliza Mzee mmoja aliyejulikana kama Makorokocho.
"Hata sielewi mume wangu kapatwa na nini jamani...sielewi mimi" mke wa John alizidisha kilio.
"Kwani imekuaje?"
"Msogelee umwangalie maana mimi sielewi.. Namwita haamki.."
"Mh!" Aliguna Mzee Makorokocho huku akimsogelea mwalimu John.
Akamtikisatikisa John akamwita lakini John hakuitika, Ingawa John alisikia kila kitu kinachoendelea ila hakuweza kuamka.
"Mh! Mama pole sana huyu tayari ametangulia mbele za haki..."
"Ati mini?"
"Ndo ivo mama chamsingi tuwapigie ndugu zake simu, taratibu za mazishi zifanywe!"
"Hapana! Mume wangu hajafa! Iweje John afe mbele yangu.. Aaah we Mungu we!!" Mke wa Mwalimu John alilia kwa uchungu sana.

Ndugu wa mwalimu John wakapigiwa simu kupewa taarifa za msiba, taratibu za mazishi zikaanza kufanywa.

                                        *******
Dorice alipotoka bwenini kwao akaongoza moja kwa moja mpaka bweni la Mapambano ambalo ndilo alilokuwa akiishi Eddy, alitembea kama mwendawazimu mpaka alipotia timu katika bweni hill bila kujali ni bweni la wavulana pekee. Dorice aliongoza mpaka kitanda cha Eddy ambapo alimkuta Eddy akiwa na wenzake watatu. Na alikuwa akiwasimulia juu ya uhusiano wake mpya na Doreen.

"Habari zenu" alisalimia Dorice akiwa amevimba kama kiboko aliyekasirishwa. Eddy hakujibu isipokuwa wale rafiki sake.
"Umefuata nini hapa we mpuuzi?"
"Nimekufuata wewe nataka nijue kama unanipenda mimi au Doreen?"
"Hivi we mwanamke unawazimu we? Nikupende wewe kama nani? Doreen ndo mpenzi wangu, nampenda sana."
"Kweli!?"
"Ndio tena niondokee hapa, unanitia kinyaa!" Eddy alimsukuma Dorice kwanguvu Dorice akaanguka chini na kujigongesha kichwa kwenye kitanda.
"Eddy usifanye ivo bhana utamuumiza mwenzio" alisema rafiki mmoja wa Eddy kwani alimuonea huruma sana Dorice.
"Achana nae mpumbavu huyo"
"Lakini kumbuka mlikotoka"
"Achana na mimi kama unampenda si umchukue!"
Maneno Yale yaliziidi kumuumiza Dorice, aliinuka pale chini akajifuta vumbi maana bweni lilikuwa na vumbi kupita kiasi.
"Sawa Eddy! Daima kumbuka sio kila king'aacho ni dhahabu... Utanikumbuka!" Alisema Dorice kwa huzuni na kutoka.

"Akukumbuke nani wewe? We boya tu huna lolote" Eddy aliropoka maneno hayo huku akiwashangaza rafiki zake kwani daima hawakujua kama Eddy angemchukia Dorice kiasi kile kutokana na mapenzi yao yalivokuwa.

"Ama kweli watu wanabadilika..!" Alisema rafiki take Eddy na kuondoka zake.

Dorice aliondoka zake mpaka bwenini kwao, akachukua begi lake dogo na kuweka vitu vyake muhimu. Isipokuwa nguo za shule na madaftari, baada ya kupaki vizuri akachukua kanga akaivaa baada ya kutoa nguo kisha akaenda bafuni kuoga.

Alipooga na kujiandaa vizuri alikaa kitandani kwake huku kila Mara akitazama SAA yake ya mkononi ambayo alipewa na Eddy enzi za mapenzi yao. Ilikuwa SAA nzuri ya Dhahabu."Ikifika SAA kumi na mbili jioni lazima nitoroke ... Siwezi kubaki hapa!" Aliwaza Dorice akiwa kitandani kwake.

Muda huchelewa sana pale unapousubiri ndivyo ilivokuwa kwa Dorice. Muda ulichelewa lakini ukafika, kigiza kilipoanza tu akachukua begi lake na kutoka bwenini. Hakuvaa nguo za shule hivyo haikuwa rahisi kugundua kama ni mwanafunzi wa pale. Taratibu akazipiga hatua ili atoroke shuleni pale.

Licha ya kwamba alisumbuliwa na maswali ya wanafunzi wenzake ila hakujali ingawa aliwapa majibu ya uongo yanayoridhisha.

Shule ya mabango ilikuwa imezingirwa na miti mingi hivyo akapita katikati ya miti hiyo ili asioneakane kirahisi. Alipokuwa anaendelea kutembea ghafla akaona kitu mbele yake akashtuka.

                                        ********
Jioni ile tulivu Eddy na Doreen walikutana kwenye mti mmoja mzuri na tulivu. Walikuwa wamekumbatiana kimahaba huku wakipeana denda za kutosha.

"Baby nakupenda sana" alisema Eddy
"Nakupenda pia ila..."
"Ila nini mpenzi?"
"Sharti la kuwa na mimi ni kwamba hutuwezi kufanya mapenzi..." Alisema Doreen.
" eh! Kwanini?"
"Tukifanya hivyo kuna kitu kitatokea kwako?"
"Mh Doreen! Mbona sikuelewi, tutaishije kama wapenzi?"
"Nivumilie tu... Ila bado nina bikra"
"Nataka niitoe bikra yako Doreen please!"
" huwezi kufanya mapenzi na mimi, pia kuna sharti lingine mbali na hilo..."
"Bby hapa siwezi kuwa na wewe bila kufanya mapenzi, siwezi! Halafu pia siwezi kukuacha au huniamini?"
Alisema Eddy akiwa amezidiwa na hamu ya mapenzi na ilikuwa kazi ngumu sana kwake kujizuia....

Itaendelea ......
RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Saba RIWAYA: Mwanafunzi Mchawi ( A Wizard Student ) - Sehemu ya Saba Reviewed by WANGOFIRA on 22:56:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.