NICK VUJICIC, MLEMAVU ANAYEISHANGAZA DUNIA






Waswahili husema haujafa haujaumbika na thamani ulichonacho utaiona baada ya kukipoteza. Ni misemo ambayo watu wengi wamekuwa wakiitumia kwa kujua au kwa kutokujua maana zake na matumizi yake kwa namna moja au nyingine.

Na ndiyo maana watu wengi huridhika na kutojali uthamani wa wenzao kwa kufikiri walipenda kuwa hivyo. Ubinafsi ni hulka ya kila mtu lakini pale unapozidi lazima kuwe na walakini wa kwanini ujipende wewe mwenyewe na kuwaacha wanyonge wakipata shida na kuangaika mitaani huku wakiwa hawana usaidizi wowote kwa sababu ya upungufu walionao.

Walemavu ni kundi la watu ambao baadhi ya watu katika jamii hawaoni kama ni kundi la muhimu kama wao walivyo. Kutokana na matukio mbalimbali yanayoripotiwa kuonyesha unyanyapaa kwa kundi hili ambalo kama likijengewa mazingira mazuri litafanya mambo ya ajabu na kuishashanga dunia.

Lakini kwa sababu ya kutowezeshwa baadhi yao wamekuwa wakiomba misaada barabarani na hata wengine kushindwa kuhudumiwa kwa sababu ya ulemavu walionao. Japo hawakupenda wala hawakutuma maombi wazaliwe au wawe walivyo bali ni majaliwa ya mwenyezi Mungu kuwawezesha.

Maana hata kwenye vitabu vya dini vimeandikwa kuwa jaribu halina budi kukwijia lakini kila jaribu loina mlango wa kutokea. Na ndio maana nafurahi kuwaona baadhi ya watu wenye ulemavu wa vioungo na wengine wenye ulemavu wa aina mbalimbali wakifanya mambo ya kustaajabisha na watu walio wazima wa viungo kubaki midomo wazi wakishangaa.

Lazima washangae kwa sababu wengi wao hawapendi kujishughulisha na kutumia akili na uwezo waliopewa na Mwenyezi Mungu. Ukimwangalia Mtoto Mirium Chirwa ambaye ni mlemavu wa macho lakini daima mchango wake hapa nchini utakumbukwa kwa kuwa muimbaji mtoto lakini akiimba nyimbo za hisia kubwa ambazo ziliwaliza baadhi ya viongozi wakubwa hapa nchini.

Lakini, kamwe mchango wa baadhi ya wanahabari walemavu akiwemo Tuma Dandi, mwandishi na mwandaaji wa vipindi kwenye moja ya Televisheni hapa nchini ambaye kila mwaka amekuwa akijinyakulia Tuzo za umahili wa uandishi wa habari ambazo utolewa na Baraza la Habari la Tanzania yaani MCT.

Hiyo ni baadhi ya michango michache tu ya watu wenye ulemavu ambao kwa hapa nchini wamefanya mambo ya kuvutia na kubadilisha mitazamo ya watu na kuwaona walemavu wanaweza ikiwa watapewa nafasi na wao kujitambua kuwa wanataka kuwa wakina nani katika dunia ya leo.

Makala hii itamwangazia Nicholas James hali maarufu kama Nick Vujicic mlemavu asiye na mikono wala miguu lakini mchango wake hautasahaulika duniani kote.

Amezaliwa mwaka 1982, na kwa sasa ana mke na watoto wawili. Ana shahada ya kwanza ya Uhasibu ambayo aliipata mwaka 2003 katika chuo Kikuu cha Griffith kilichopo nchini humo. akiwa na umri wa miaka 20 tu.

Kamwe hajawahi kujutia Hali aliyozaliwa nayo na amefanya mambo makubwa ambayo hadi leo walio na mikono na viungo vyote vya mwili wameshindwa kuyafanya.

Hapa ndipo msemo wa wahenga kuwa kamwe Mungu akunyimi vyote ndipo unaweza kuuelewa maana tofauti na wengine wanaobaki kuombamsaada barabarani. Nick aliamua kujifunza komputa na kutumia akili yake kuwaelimisha wengine kupitia uwezo wake aliopewa wa kiuandishi.


Baadhi ya vitabu ambavyo ameviandika ni pamoja na Life without Limit: Inspiration for ridiculously, ambacho kinaelezea maisha yake na mafanikio yake. Pia kinahamasisha watu kutokata tama maana yeye alikubaliana na hali aliyozaliwa nayo.


Lakini kamwe hakukubali kuzidiwa na mwanadamu wengine anaeleza kuwa anajiona hana upungufu wowote maana hayakuwa mapenzi yake kuzaliwa hivyo bali bali ni mpango wa Mungu kumfanya alibvyo ili atumie kile alichonacho.

  Pia ameandika pia kitabu cha Stand strong: you can overcome, The Power of Unstoppable Faith: Your Keys to a Fulfilled Life, Attitude is Everything: The story of an extraordinary life, Unstoppable: The Incredible Power of Faith in Action. Na vingine vingi ambavyo ukipata kuvisoma hautobaki kama ulivyo.

 

Naipenda nukuu moja ya Nick ambayo ameiandika kwenye kitabu chake cha The power of Unstoppable Faith ambapo anasema

 

“People often ask me how I stay positive and where I find the strength to overcome my disabilities. My answer, always, is ‘I pray for God’s help and then exercise unstoppable faith”

 

Akiwa na maana ya kwamba watu wanamuuliza ni kwa jinsi gani amekuwa na mafanikio makubwa huku ni mlemavu, na yeye huwajibu kuwa ni msaada wa maombi anayoomba kwa Mungu na kuwa na imani iliyo kuu.

 

Katika maisha ya Nick kamwe neno kushindwa kwake alipo maana kila kitu anafanya mwenyewe pasipo kutegemea msaada wa mtu mwingine. Kama yeye ameweza kwa nini wewew ushindwe? Jiulize una mikono mingapi, miguu na akili kiasi gani ambayo Muumba wako amekupa na uutumie kubadili maisha yako na kuandika historia duniani.

 

Nick si muandishi tu ameenda mbali zaidi pia ni muigizaji aliyepata kuigiza na kuvuma katika filamu ikiwemo ile ya The butterfly Circus na The lost Sheep, ambapo mwaka 1990 alishinda tuzo ya The Australian young citizen Award, tuzo ambayo utolewa na serikali ya Australia kutambua mchango wa vijana waliofanya mambo ya kipekee nchini humo.

 

Pia alishinda tuzo ya mwiigizaji bora katika filamu ya the butterfly circus ambayo ilirekodiwa mwaka 2010 huku ikiwashirikisha zaidi ya waigizaji 150. Filamu hii ilielezea maisha ya wamerekani katika miaka ya 1930 kwenye kipindi cha udololo wa uchumi Nchini Marekani tatizo lililosababisha kuongezeka kwa utegemezi mkubwa kwa taifa na vijana wengi kukosa ajira nchini humo.

 

Hivyo basi ni rai yangu kwa watanzxania wote kufanya kazi kwa kujituma kama kauli mbiu ya Rais wa awamu ya Tano kuwa watu wafanye kazi maana ni muda wa Hapa kazi Tu. Na kamwe usikubali kushindwa maana kila kitu kinawezekana ikiwa utatia juhudi na moyo wa kukifanya.

Mwandishi wa makala haya ni mwanafunzi kutoka shule Kuu ya Uandishi wa Habari na mawasiliano kwa Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Anapatikana kwa mawasiliano ya 0763580901

NICK VUJICIC, MLEMAVU ANAYEISHANGAZA DUNIA NICK VUJICIC, MLEMAVU ANAYEISHANGAZA DUNIA Reviewed by WANGOFIRA on 20:26:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.