MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA SHEREHE ZA JUBILEE KANISA LA WAADVESTA WASABATO KIRUMBA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh John Mongella,Juni 30,2016 amezindua Sherehe za Jubilee ya Miaka 50 ya injili jiji la Mwanza katika kanisa la Waadventista Wasabato Kirumba Mwanza Tanzania. Mkuu huyo katika hotuba yake, amelipongeza kanisa la Kirumba kuwa na jubilee ya miaka 50 Lakini pia amelipongeza kwa huduma ya malezi ya vijana wa kanisa hilo wakingali wadogo na kwamba kwa kufanya hivo ni kuliandaa kanisa na Taifa kwa ujumla kuwa na viongozi waadilifu. Mkuu huyo wa Mkoa pia ameyataka madhehebu ya dini yawe mstari wa mbele katika kukemea maovu ili Taifa letu lidumu kuwa na Amani aidha amewasihi waumini kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania. Miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria Hafra hiyo ni, Wachungaji wastaafu wa kanisa la Waadventista Wasabato, Familia asisi za kanisa la Kirumba linalosheherekea miak,Mh Diwani wa Kata ya Kirumba Mwanza, Mh Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Kirumba Bondeni, waumini wa kanisa,wananchi majirani katika eneo la Kirumba, watu mashuhuri , na viongozi wa vyama vya siasa,ndugu jamaa na marafiki; Bila kumsahau Prof na Mchungaji Leal Caesar kutoka Makao Makuu ya kanisa la Waadventista Wasabato nchini Marekani. Katika ziara hiyo Mh. Mkuu wa Mkoa alipata nafasi ya kutembelea mabanda ya maonesho ya kazi za mikono,Ufunuo Publishing House, Banda la historia na kumbukumbu za kanisa akiongozwa na mwenyeji wake mchungaji Sadoki Butoke Askofu Mkuu wa Jimbo La Nyanza Kusini( South Nyanza Conference)katika kanisa hilo, Pia alipata nafasi kuona shughuli za huduma za afya ambazo zimeendelea kwa siku 5 mfululizo bure.Huduma ya utoaji damu kwa kujitolea ilikuwa ikiendelea. Imetaarifiwa kwamba, huduma hizo za afya zimehudumia watu wapatao 900 hadi mchana wa siku ya juni 30,mwaka huu.

Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ

MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA SHEREHE ZA JUBILEE KANISA LA WAADVESTA WASABATO KIRUMBA MKUU WA MKOA WA MWANZA AZINDUA SHEREHE ZA JUBILEE KANISA LA WAADVESTA WASABATO KIRUMBA Reviewed by WANGOFIRA on 23:54:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.