Mkapa Awataka Watanzania Kufanya kazi kwa Bidii Na Kupunguza Lawama


Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin William Mkapa amewataka watanzania kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa bidii na kupunguza lawama ili kuonyesha uzalendo aliouacha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais Huyo Mstaafu ameyasema hayo katika mkutano wa nane wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere ambao umefanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na kuongeza kuwa watanzania wengi wamekua na desturi ya kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali badala ya kufanya kazi kwa maendeleo ya nchi.

"Watanzania tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii ili tuifikishe nchi yetu Kwenye maendeleo na si kutumia muda mwingi Katika kuilaumu serikali " alisema Dkt Mkapa.

Aidha Dkt. Mkapa amesema kuwa ili uzalendo uwepo tunatakiwa kutumia vizuri uhuru wa kuongea Katika kuleta maendeleo na si kuleta uchochezi Katika nchi na kusababisha uvunjifu wa amani ambayo ameiacha Mwalimu Nyerere.

Mbali na mkutano huo pia kulikua na uzinduzi wa kitabu cha uchumi wa kisiasa wa mabadiliko ya Tanzania kijulikanacho kama (political economy of change in Tanzania) ambacho kina lengo la kukuza uchumi na siasa nchini.

Mkutano huo wenye lengo la kudumisha uzalendo na kukuza uchumi nchini umehudhuriwa na wawakilishi Mbali Mbali wa kitaifa na kimataifa wakiwemo baadhi ya mabalozi na wanazuoni kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wa Makamu mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Prof. Rwekaza Mukandala alisema kuwa mkutano huo unalenga kudumisha na kuendeleza aliyoyaacha Baba wa Taifa Hayati Mwl. J.k Nyerere.

Mbali na hayo amewataka vijana na watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi na kuendeleza ujamaa aliouacha Mwalimu.
Mkapa Awataka Watanzania Kufanya kazi kwa Bidii Na Kupunguza Lawama Mkapa Awataka Watanzania Kufanya kazi kwa Bidii Na Kupunguza Lawama Reviewed by WANGOFIRA on 20:10:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.