Milioni 800 Zatengwa Kuwasaidia Waathirika wa UKIMWI Nchini
ZAIDI
ya Sh milioni 800 zinatarajiwa kukusanywa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita
(GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS)
kwa ajili ya kusaidia waathirika wa Virusi Vya Ukimwi mwaka huu.
Fedha
hizo zitakusanywa kupitia kampeni maalumu ya kupanda mlima Kilimanjaro
ijulikanayo kama Kill Challenge inayofanyika kwa mwaka wa 15, ambayo kwa
mwaka huu wapanda mlima 100 wamejitokeza kushiriki.
“Mgodi
wa Geita kwa kushirikiana na Tacaids unatarajia kupandisha watu 50
katika kilele cha mlima Kilimanjaro na kundi lingine la waendesha
baiskeli 50 linataraji kuzunguka mlima huo kwa ajili ya kukusanya fedha
hizo,” alisema Meneja Mawasiliano wa Mgodi wa GGM, Tenga Tenga.
Tenga
alisema kampeni hiyo ya Kili Challenge inaongozwa na Balozi wake,
Mrisho Mpoto ambaye ni msanii wa kughani mashairi na upandaji huo wa
mlima utafanyika Julai 16 na kumalizika Julai 22, mwaka huu.
Alisema
mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa Awamu
ya Nne, Jakaya Kikwete, ambaye ataanzisha safari hiyo huku mapokezi ya
kuwapokea wapandaji hao akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky
Sadiki.
Naye
Mwakilishi wa Tacaids, Jackson Peter, alisema Kili Challenge ya mwaka
huu imepata uzito wa kipekee kutokana na Umoja wa Mataifa (UN) kupitia
Shirika lake la Maendeleo la (UNDP) kutoa wawakilishi wanane kushiriki
upandaji mlima huo kwa ajili ya kusaidia watu walioathirika na Virusi
Vya Ukimwi nchini.
Balozi
wa Kili Challenge, Mpoto aliwataka wananchi na jamii kwa ujumla
kutambua mapambano dhidi ya Ukimwi ni ya jamii yote hivyo inapaswa
kuunga mkono jitihada za serikali kwa ajili ya kupambana ili kufikia
sifuri tatu.
“Naamini
kwamba jitihada zinazofanywa na mfuko huu zinahitaji kuungwa mkono na
Watanzania wote na wadau wenye machungu na nchi hii, hivyo tuungane kila
mmoja wetu ama kwa kuxchangia au kumuelisha mwenzake ili mapambano haya
yalete mabadiliko,” alisema Mpoto.
Tangu
kuanza kwa kampeni hiyo miaka 15 iliyopita zaidi ya Dola za Marekani
8,000 zimekusanywa na kugawiwa katika asasi mbalimbali nchini
zinazoshiriki katika mapambano na kusaidia waathirika wa Ukimwi.
Fedha
hizo zimepelekwa katika kusaidia mapambano dhidi ya Ukimwi, ikiwamo
kujenga vituo vya ushauri na upimaji wa Ukimwi, ambavyo baadhi yao ni
vile vilivyopo mkoani Tanga, Manyoni mkoani Singida na Geita.
Milioni 800 Zatengwa Kuwasaidia Waathirika wa UKIMWI Nchini
Reviewed by WANGOFIRA
on
23:30:00
Rating:
No comments: