Milioni 140 za serikali ya wanafunzi UDSM kupangiwa matumizi Leo



Bajeti ya Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) 2016/2017 inatarajia kusomwa, kujadiliwa na kupitishwa au kukataliwa na bunge la DARUSO siku ya kesho Jumamosi kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa saba mchana.

Bajeti hiyo itawasilishwa bungeni na Waziri wa fedha  na uwekezaji DARUSO, Jackline Kavishe kabla ya kujadiliwa na wabunge wote.

Jumla ya fedha milioni 140 zinatarajiwa kupangiwa matumizi kwa mwaka 2016/2017 huku zaidi ya wabunge 130 wakitarajiwa kushiriki mjadala wa bajeti hiyo.

Iwapo bajeti hiyo itapitishwa na bunge itakuwa ni rekodi ya aina yake kwa serikali mpya ya DARUSO chini ya Rais Erasmi Leon kwani kwa miaka miwili iliyopita bajeti ya serikali ya wanafunzi imekuwa ikikataliwa na bunge katika uwasilishaji wake wa mara ya kwanza.
Milioni 140 za serikali ya wanafunzi UDSM kupangiwa matumizi Leo Milioni 140 za serikali ya wanafunzi UDSM kupangiwa matumizi Leo Reviewed by WANGOFIRA on 17:21:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.