MAKONGORO MAHANGA MWENYEKITI MPYA WA CHADEMA MKOA WA ILALA.


Kufuatia uchaguzi mdogo uliofanyika ili kuziba nafasi za uongozi katika Mkoa maalum wa kichama wa Ilala, yafuatayo ni matokeo ya uchaguzi huo:

*Nafasi ya Mwenyekiti*

1. Makongoro Mahanga kura 14
2. Adolf Mkono kura 11
3. Thomas Nyahende kura  7
4. Wengine wanne kura 0

*Nafasi ya Katibu*

1. Amani Antony Mgheni kura 13
2. Clemence Kambangwe kura 09
3. Lilian Masiaga kura 05
4. Goodluck Kagande kura 05
5. Lucas Maira kura 00


Nafasi ya Mwenyekiti kura zimerudiwa kupigwa ambapo Dk. Mahanga (mshindi wa kwanza) na Adolf Mkono (mshindi wa pili) ili mshindi apatikane kwa zaidi ya 50% kama utaratibu unavyoelekeza.
Matokeo katika upigaji kura wa mara ya pili;


1. Dk. Makongoro Mahanga kura 23
2. Adolf Mkono kura 08


Msimamizi wa Uchaguzi huo, Bernard Mwakyembe ambaye ni makamu mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya Chadema Greater Dar es Salaam amewatangaza Dk. Makongoro Milton Mahanga kuwa Mwenyekiti Mpya wa Chadema Mkoa wa kichama Ilala huku akimtangaza Amani Antony Mgheni kuwa Katibu.
MAKONGORO MAHANGA MWENYEKITI MPYA WA CHADEMA MKOA WA ILALA. MAKONGORO MAHANGA MWENYEKITI MPYA WA CHADEMA MKOA WA ILALA. Reviewed by Unknown on 08:53:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.