MAELEZO JUU YA KUOMBA MKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017Bodi ya mikopo tayari imetangaza kufungua dirisha la maombi Kwa waombaji wote wa mikopo, kuanzia tar 27/juni 2016 hadi tar 31 julai 2016.

Maombi ya mkopo yanafanywa na mwanafunzi ambaye hadhaminiwi na anufaiki na mkopo huo kutoka bodi wala shirika lolote.

Mwanafunzi huyo awe amemaliza kidato cha Sita Kati ya mwaka 2014 na 2016. na asiwe ameajiriwa.

Pia mwanafunzi huyo anapaswa awe mtanzania,kama sheria no. 9 ya 2004. ya bodi.

Lazima mwanafunzi aombe ONLINE, kupitia OLAS yaani (online loan application system). Baada ya kuwa umenunua vocha ya shilingi 30000/=.M-PESA unaingiza namba zile za vocha. ulizonunua M-PESA.

Unaanza jaza details kadhaa online, kama matokeo, mahali unapoishi, kazi ya baba, mama, Jina la mdhamini, anapoishi, n.k

Ukimaliza una print fomu zile,  unaziambatanisha na na nakala zifuatazo.

*nakala ya cheti cha kuzaliwa
* nakala ya cheti cha kidato cha nne.
*nakala cheti cha kifo kama mzazi /wazaz wamekufa.
*nakala ya barua ya daktari kama mzazi ni mgonjwa au mlemavu.
*>nakala ya barua ya kustaafishwa kama mzazi, mlezi, Hana kazi au amestaafu
>nakala ya kitambulisho cha mdhamini. Hasa cha uraia au cha mpiga kura.
>passport size yako na ya mdhamini wako.

Baada ya hapo unapeleka Kwa mwanasheria anayetambulika, aidha wakili au hakim. Kuna sehemu yake ya kujaza pia kupiga mhuri na saini yake katika kila nakala ulioiambatanisha ili kuthibitisha.

Baada ya hapo nenda Posta katume Kwa njia ya EMS.

MAELEZO YA ZIADA.

Mkopo unaotolewa unajumuisha yafuatayo.
>meals and accommodation
>tuition fees
>books and stationary
>special faculty
>field and training
>research expenses

Kwa CONTINUOUS STUDENTS, yeyote anaye nufaika na malipo yeyote hapo,hata kama ni 0% huyo hapaswi kuomba Tena mkopo.

Bali mtu wa namna hiyo anapaswa asubiri akate rufaa Kwa kuomba aongezewe kiasi cha fedha, anaweza akawa analipiwa meals and accommodation tuu, anapaswa aombe aandike sababu Za msingi, na Za mashiko wakati wa kukata rufaa (appeal).

Hivyo yeyote ambaye anadhaminiwa na bodi hata kama ni kidogo, asifanyi maombi asubiri Muda wa kukata rufaa. Ambapo tutafahamishana pia.

Shukrani saana, ninawaomba wote ambao hamjawahi fanya maombi au mlifanya mkakosa, msikati tamaa.

Kwa muongozo zaidi tembelea tovuti ya bodi ya mikopo
Soma hapa
MAELEZO JUU YA KUOMBA MKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 MAELEZO JUU YA KUOMBA MKOPO KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017 Reviewed by Unknown on 22:06:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.