KIKWETE ATEULIWA KUWA BALOZI WA HESHIMA
Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya
nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea barua ya uteuzi kutoka kwa Prof.
Kamuzora alipofanya ofisi za CCM Lumumba
Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya
nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Prof. Kamuzora alipofanya
ofisi za CCM Lumumba
KITUO cha Ufundi cha
Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for Agricultural and
Rural Cooperation, CTA) kilicho chini ya Umoja wa Ulaya (EU) chenye
makao makuu mjini Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais Mstaafu Dk. Jakaya
Kikwete kuwa Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya
Kilimo katika Mabara ya Afrika, Karibiani na Pacific.
Katika barua iliyokabidhiwa na
mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora, CTA wameainisha kuwa Dk.
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, ameteuliwa kwa kutambua
mchango na juhudi zake katika kukiendeleza kilimo nchini Tanzania na
barani Afrika.
Katika
wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk. Kikwete aweze kuiwakilisha
katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umuhimu wa
kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha na
uhakika kwa vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani
na Pasifiki. Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.
Dk.
Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika
kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidiana na taasisi hiyo ambayo ni
ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani
na Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelgiji.
Prof.
Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya
CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano
tangu 2013 hadi 2018.
KIKWETE ATEULIWA KUWA BALOZI WA HESHIMA
Reviewed by WANGOFIRA
on
20:46:00
Rating:
No comments: