Halmashauri nchini zatakiwa kufanya kazi kwa weledi na ufanisi ili kuleta matokeo chanya na kwa wakati, huku wakijiepusha na ufujaji rasilimali za umma wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikaliza Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe alipokuwa akimwakilisha Waziri wa nchi OR – TAMISEMI Mhe. George Simbachawene katika uzinduzi rasmi wa mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized Climate Finance in Tanzania) jana mjini Dodoma.

“Niseme tu kuwa nategemea utendaji wenye matokeo chanya kwa kufanya hiyvo kutajenga imani kwa wafadhili, Wakurugenzi wote nchini fanyeni kazi kwa weledi,ufanisi na muepuke kufuja mali za umma” Alisema Mhandisi Iyombe.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized Climate Finance in Tanzania) jana mjini Dodoma.

Mhandisi Iyombe aliongeza kuwa mradi huu umelenga kuwajengea uwezo wanajamii katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi ambapo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika kukabiliana na hilo.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo hususan Shirika la Kimataifa la Mazingira na Maendeleo (IIED), Haki Kazi Catalyst (HKC), Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) chini ya ufadhili wa Serikali ya Uingereza (UK-aid) na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo (UNCDF LoCAL) itatekeleza mradi huu katka Halmashauri 15 nchini.

Halmashauri hizo ni pamoja na Kondoa, Bahi, Manyoni, Mpwapwa, Kiteto, Same, Simanjiro, Kilwa, Siha, Mbulu, Iramba na Pangani ambazo zimejumuishwa na Halmashauri za Monduli, Ngorongoro na Longido zilizokuwa katika mradi wa majaribio.

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Dkt. Deo Mtasiwa
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Dkt. Deo Mtasiwa akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized Climate Finance in Tanzania) jana mjini Dodoma.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu anyeshughulikia Afya kutoka OR-TAMISEMI Deo Mtasiwa amesema kuwa kwakuwa Serikali tayari imekwisha tengeneza mfumo imara ilikuhakikisha utekelezaji wa mradi huo unafanikiwa kuanzia ngazi ya kijiji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huu MwakilishiMshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED) Alais Morindat alisema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa siyo kitu kipya na kuongeza kuwa historia ya mradi huo inatokana na athari zilizojitokeza katika jamii za wafugaji katika maeneo ya Kasikazini mwa Tanzania ambapo mifugo mingi katika maeneo ya Monduli, Ngorongoro na Longido ilipoteza uhai.

Meneja Miradi wa Mfuko wa Umoja wa Taifa wa Maendeleo (UNCDF) Bw. Fakri Karim
Meneja Miradi wa Mfuko wa Umoja wa Taifa wa Maendeleo (UNCDF) Bw. Fakri Karim akiwasilisha mada namna mfuko wao unavyoshiriki katika mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized Climate Finance in Tanzania) wakat wa uzinduzi wa mradi huo mjini Dodoma.
MwakilishiMshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED)  Alais Morindat
MwakilishiMshauri wa Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo (IIED), Alais Morindat akielezea chimbuko la mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized Climate Finance in Tanzania) wakati wa uzinduzi wa mradi huo mjini Dodoma.
Baadhi ya wadu wadau wa mradi wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia
Baadhi ya wadu wadau wa mradi wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi akiwemo mwakilishi wa mtandao wa wanahabari watoto wanaoshughulika na mabadiliko ya tabia nchi Bi. Getrude Clement (16) mwenye tisheti ya kijani wakifuatilia mada wakati wa uzinduzi wa mradi huo leo mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe (watano kutoka kushoto)
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe (watano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika uzinduzi wa mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabia nchi (Decentralized Climate Finance in Tanzania) mjini Dodoma. (Picha na: Nasra Mwangamilo, TAMISEMI).