TODAY IS A BEAUTIFUL DAY BUT I CAN NOT SEE IT/ UZURI WA LEO SIWEZI KUONA


Waswahili usema ukitaka kuona umuhimu wa ulichonacho kipoteze, ungana na WANGOFIRA BLOG kuchangia japo kiasi kidogo tu, ili kufanikisha matibabu ya Bernadetha Msigwa ( mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya Rasilimali watu na Utawala( HUMAN  RESOURSES MANAGEMENT) Katika chuo kikuu cha Mzumbe. Aliyepata ulemavu wa macho hivi karibuni  na kwa sasa amekuwa KIPOFU ana kupoteza uwezo wa macho yake kuona tena.

Bernadetha anahitaji msaada wako wa hali na mali, maana kwa sasa anateseka kuikabili hali ambayo kiukweli hajaizoea. 

Alizoea kufanya mambo yake pasipo kuwa na usaidizi lakini kwa saas hawezi bila ya kuwa na msaidizi. Jifikirie anapata shida na kuumia jinsi gani, alizoea kuona uumbaji wa Mungu lakini sasa hawezi tena.

Alizoea kwenda kufurahi na kushangilia na ndugu, jamaa, rafiki , na pengine na boyfriend wake, lakini kwa sasa hawezi kuyafanya yote hayo hawezi yafanya bila ya usaidizi.

Jifikirie na uweke akilini mwako kuwa ni mwanao au dadako, ndugu au jamaa ungefanyaje ili aweze kurudia hali yake ya kawaida na aliyoizoea. 

KUTOKANA NA HALI HIYO JUMUIYA YA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA MZUMBE WAMEONA NI VYEMA KUFANYA FUNDRAISING (CHANGIZO LA WAZI) SIKU YA JUMAMOSI KUANZIA SAA 2:00 Hadi saa 6:oo usiku , KATIKA UKUMBI WA SAMORA.

Kwa Uliyeguswa na mkasa huu mtumie Chochote Ulichonacho kwa

M-PESA  0766-563 854 Au TIGO PESA  Namba 0656-731-487 jina ni BERNADETHA MSIGWA.

Hii hapa ni Barua yake fupi kwa watanzania na wengine wote mtakaoguswa kumsaidia, Pia Maombi yenu ni ya Muhimu sana ili Mwenyezi Mungu amsaidie arejee kwenye hali yake ya kawaida.

MUNGU AWABARIKI MNAPOTAFAKARI JINSI YA KUMSAIDIA.



TODAY IS A BEAUTIFUL DAY BUT I CAN NOT SEE IT/ UZURI WA LEO SIWEZI KUONA TODAY IS A BEAUTIFUL DAY BUT I CAN NOT SEE IT/ UZURI WA LEO SIWEZI KUONA Reviewed by WANGOFIRA on 05:24:00 Rating: 5
Powered by Blogger.