POLISI WANASWA KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA YA 7.2 MIL


 
POLISI mkoani Rukwa inawashikilia askari wake wawili wa Kituo Kikuu cha Polisi wilayani Nkasi, wakituhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh milioni 7.2 wamsaidie mtuhumiwa. 

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Rukwa, Leonce Rwegasira alitaja askari hao kuwa ni Konstebo Filbert Ruhemeja na Konstebo Bahati Sengerema, ambao walikuwa wakifanya kazi katika Kituo cha Polisi mjini Namanyere wilayani Nkasi. 

Alisema polisi inawafanyia uchunguzi wa kina askari wake wawili, wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kuomba rushwa ya Sh milioni 7.2 na iwapo watabainika halitasita kuwatimua na kuwafikisha mahakamani. 

Rwegasira alisema hayo jana ofisini kwake wakati anazungumza na mwandishi wetu alipotaka kujua ni hatua gani zilizochukuliwa dhidi ya polisi hao kutokana na kuwepo kwa tuhuma hizo za kuomba na kupokea rushwa. 

Alisema askari hao wawili wa polisi, wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa ya fedha kutoka kwa mtu mmoja ili wamsaidie katika shitaka linalomkabili.
POLISI WANASWA KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA YA 7.2 MIL POLISI WANASWA KWA KOSA LA KUOMBA RUSHWA YA 7.2 MIL Reviewed by WANGOFIRA on 21:33:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.