NANI YUPO NYUMA YA WAWINDAJI HARAMU HAWA?

[​IMG]Kuna mambo yanashangaza kidogo ila yanasikitisha sana ukiyaangalia. Tunazo mamlaka zetu, tumeziamini na zinatakiwa kuwajibika kwetu kama watanzania na kulinda rasilimali zetu.Kampuni ya Green Mile ilifungiwa lakini ajabu ni kuwa wanaendelea kutamba Tanzania yetu.

Kinachosikitisha, mawakili/watetezi wa wauaji hawa ni watanzania Namwona hadi Ndg. Mwitumba (aliwahi kuwa IPP Media nadhani gazeti la ThisDay) kwenye picha hii. Hata kama ni pesa, uzalendo urudi na tuone hatari inayolikabili Taifa letu.

Kifupi, habari kuhusu kampuni hii hazijaanza leo na nakumbuka Msigwa alipiga sana kelele 2014. Ni nani aliwarudishia leseni waarabu hawa?


[​IMG]

VIDEO inayosikitisha:


Mataifa mengine yanatushangaa, soma: Leaked Animal Abuse Video Shows Everything That's Wrong with Big Game Hunting

Aidha, SHERIA YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI NAMBA 5 YA MWAKA 2009 ina ufafanuzi wa wazi kabisa juu ya vitendo vya kihalifu kama hivi (nimeambatanisha PDF version yake).

Wanaua hadi ndege ambao wanapatikana Tanzania pekee, wanataka tuwaachie nini wajukuu zetu?

Kumgonga mnyama na gari ni uwindaji huu?

[​IMG]

===

The video is apparently a promotional tool for Green Mile and features “highlights” from the United Arab Emirates-based company’s 2012 hunting season. Highlights include shooting wildlife from moving jeeps, running over a baby gazelle with a jeep, letting young children shoot at animals and capturing a baby zebra and holding it while it cries. The hunters regularly watch animals writhe and slowly die, and animals are chased with trucks and shot at from close range.

These abuses were revealed in March 2014, but being well-connected politically, Green Mile kept its hunting license until July when Tanzania’s Minister of Natural Resources and Tourism, Lazaro Nyalandu finally revoked the company’s permission to hunt.

===

Magufuli tusaidie, nani aliwarudishia leseni watu hawa? Serikali iliyopita ilipigwa dongo kuwa imefumba macho Tanzania ikipoteza idadi kubwa na wanyama na gazeti la Guardian la UK - Tanzania turns a blind eye to poaching as elephant populations tumble

Ni matumaini yangu kuwa tunazinusuru mbuga zetu na wawindaji majangili kama hawa.


CHANZO JAMII FORUM
NANI YUPO NYUMA YA WAWINDAJI HARAMU HAWA? NANI YUPO NYUMA YA WAWINDAJI HARAMU HAWA? Reviewed by WANGOFIRA on 21:01:00 Rating: 5
Powered by Blogger.