Mtoto Wa Miaka 7 Atupwa Msituni na Wazazi Wake Kwa Kupiga Mawe Gari la Jirani

Adhabu ni sehemu ya maisha katika malezi ya watoto lakini imekuwa tofauti kwa wazazi hawa kutoka Japan ambao waliamua kumuadhibu mtoto wao mwenye umri wa miaka (7) Yamato Tanooka, kwa kumuacha katika msitu wa kisiwa cha Hokaido ambapo ni makazi ya wanyama pori baada ya kumkuta na kosa la kurushia mawe magari yaliyokuwa jirani yao.



Kikosi cha waokoaji zaidi ya 150 bado kinaendelea na msako huko Nanae Japan ikiwa leo ni siku ya tatu tangu apotee. Wazazi wa mtoto huyo wamekiri kufanya hivyo ila haikuwa dhumuni lao kumuacha kwa muda mrefu kwani walirudi eneo la tukio muda mfupi tangu wamuache ila walipofika hawakumkuta.



Mwanzoni baba wa mtoto huyo aliripoti kupotea kwa mwanae walipokuwa wanatafuta mboga, lakini baadae akaamua kuwaambia polisi ukweli na kusema walimshusha kwenye gari kama kumpa adhabu tu. Mpaka sasa polisi wanafikiria juu ya swala hili na huenda wakafunguliwa kesi ya ‘Utelekezaji wa mtoto‘.
Mtoto Wa Miaka 7 Atupwa Msituni na Wazazi Wake Kwa Kupiga Mawe Gari la Jirani Mtoto Wa Miaka 7 Atupwa Msituni na Wazazi Wake Kwa Kupiga Mawe Gari la Jirani Reviewed by WANGOFIRA on 20:23:00 Rating: 5
Powered by Blogger.