MCHUNGAJI ANASWA NA PEMBE ZA NDOVU ZIKIWA ZIMEFICHWA KANISANI

NB-Siyo Meno yaliyokamatwa

Jeshi la Polisi Mkoani Katavi kwa kushirikiana na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wamemkamata mchungaji wa Kanisa la Moravian Kata ya Usevya Tarafa ya Mpimbwe wilaya ya Mlele akiwa na mtu mmoja ambao wajina yao yamehifadhiwa wakiwa na meno ya tembo 11 yenye thamani ya shilingi milioni 90 wakiwa wameyahifadhi ndani ya kanisa. 

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Damas Nyanda aliwaambia waandishi wa Habari jana ofisini kwake kuwa watuhumiwa hao walikamatwa juzi majira ya saa mbili na nusu katika Kanisa la Moraviani ililoko katika Kijiji cha Usevya. 

Alisema Mchungaji huyo wa Kanisa la Moravian akiwa na mwenzake mmoja ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi walikamatwa kufuatia taarifa zilizolifikia Jeshi la Polisi na kwa Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi kuwa watu hao wanajihusisha na biashara  haramu ya meno ya tembo na wamekuwa wakiyahifadhi ndani ya kanisa. 

Baada ya taarifa hizo polisi na TANAPA walianza kufanya uchunguzi kuhusiana na taarifa hizo walizozita kutoka kwa raia wema hukusiana na tuhuma za biashara hiyo haramu ya meno ya tembo. 
 
Kamanda Nyanda alieleza ndipo jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Askari wa Tanapa walipoweza kufika katika Kanisa la Moroviani Usevya na kufanya upekuzi ndani ya Kanisa hilo. 

Katika upekuzi huo waliweza kukamata meno ya Tembo vipande 11 yenye uzito wa kilogramu 20.3 yenyethamani ya shilingi Milioni 90 yakiwa yamehifadhiwa ndani ya tenga la kubebea mizigo yakiwa yamehifadhiwa ndani ya Kanisa la Moroviani Usevya lililokuwa likiongozwa na mchungaji huyo anaeshikiliwa na Polisi. 

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi alisema katika matukio mengine mawili tofauti yaliotokea Mei 8 majira ya saa mbili usiku huko Katika maeneo ya Mgolokani Kata ya Sitarike Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Polisi kwa kushirikiana na Askari wa Hifadhi ya Katavi walimkamata mtu mmoja ambae jina lake limehifadhiwa akiwa na jino moja la Tembo ..

Kwa mujibu wa Nyanda mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya Askari kufanya upekuzi ndani ya nyumba yake mtuhumiwa na ndipo walipo weza kukamatwa na jino moja la Tembo likiwa limefifadhiwa ndani ya nyumba yake . 

Tukio la pili lilitokea siku hiyo hiyo katika maeneo ya Mgolokani Kata ya Sitalike ambapo mtu mmoja ambae nae jina lake limehifadhiwa kwa ajiri ya upelelezi alikamatwa akiwa na jino moja la Simba akiwa amerihifadhi ndani ya nyumba yake. 

Mtuhumiwa alikamatwa baada ya kufanyika upekuzi ndani ya nyumba yeke na ndipo alipokamatwa akiwa na jino moja la samba akiwa amehifadhi ndani ya nyumba yake 

Kaimu Kamanda Damas Nyanda alisema watuhumiwa wote waliokamatwa kwenye matukio hayo wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma zinawazowakabili. 

Ametoa wito kwa wananchi wanaojihusisha kufanya biashara haramu za magendo kama vile uharibifu wa rasilimali za taifa mfano vitendo vya ujangili uwindaji haramu kuacha mara moja na badala yake wafanye shughuli halali katika kujipatia kipato chao.
MCHUNGAJI ANASWA NA PEMBE ZA NDOVU ZIKIWA ZIMEFICHWA KANISANI MCHUNGAJI ANASWA NA PEMBE ZA NDOVU ZIKIWA ZIMEFICHWA KANISANI Reviewed by WANGOFIRA on 20:45:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.