Bodi ya TCU yavunjwa kutokana na kupitisha majina ya wanafunzi wasiokuwa na vigezo.
Serikali
imievunja bodi ya tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) huku mwenyekiti wake
Hawadhi Mang’enywa ambaye mamlaka ya uteuzi wake yanatokana na rais John
Pombe Magufuli akiridhia asimamishwe kazi baada ya kubainika bodi hiyo
kupitisha majina ya wanafunzi 486 kusoma shahada ya ualimu chuo kikuu
cha mtakatifu Joseph kampasi ya Arusha na Songea huku wakiwa hawana
vigezo na baadhi yao wakinufaika na mikopo ya elimu ya juu.
Waziri wa elimu sayansi na teknolojia Joyce Ndalichako amesema
uamuzi huo umefikiwa baada ya wanafuzni waliokuwa wakisoma katika chuo
hicho kuhamishwa katika vyuo vingine na kubainika kuwa hawana uwezo
ndipo uchunguzi juu yao ukafanyika ambapo kati yao 486 walibainika elimu
yao kuwa ya kidato cha nne na ufaulu wao ukiwa juu ya alama 32 ambao
hawastahili hata kusomea fani hiyo kwa ngazi ya cheti.
Kufuatia bodi hiyo ya TCU kuvunjwa huku shughuli zake ziendelee
kufanya kazi ikiwemo udahili wa wanafunzi Mhe Ndalichako amewateua kwa
muda Profesa Eliuther Mwageni kukaimu nafasi ya katibu mtendaji na
Kokubelwa Katunzi Mollel kumaimu nafasi ya ukiurugenzi wa udahili na
nyaraka.
Aidha Mhe Ndalichako ametumia nafasi hiyo kubainisha kuwa wizara
imebaini uwepo wa wanafunzi hewa katika vyuo vikuu nchini ambao wamekuwa
wakichukua fedha za mikopo ya elimu ya juu kinyume na taratibu ambapo
hatua kali zitachukuliwa kwa chuo chochote kitakachobainika kuhusika na
mchezo huo mchafu.
Bodi ya TCU yavunjwa kutokana na kupitisha majina ya wanafunzi wasiokuwa na vigezo.
Reviewed by Unknown
on
22:54:00
Rating: