BADO HAKIJAELEWEKA UDSM, WANAFUNZI WAGOMA KUINGIA MADARASANI WATAKA WAINGIZIWE PESA ZA BOOM

 

 Wanafunzi wa chuo kikuu cha UDSM wamegoma kuingia madarasani kuanzia leo mpaka pale bodi ya mikopo iingize pesa za kujikimu kwenye akaunti zao. Wanafunzi hao wamedai kuwa ni wiki ya kumi, lakini bado hawajaingiziwa pesa zao ukiachilia mbali kusaini pesa hizo.

Mgomo huo umeanza jana usiku baada ya Rais wa wanafunzi Leon Erasmi kuwatangazia wanafunzi kutoingia madarasani hadi bodi ya mikopo watakaapowaingizia pesa za kujikimu kwenye akaunti zao.

Hali hiyo imetokea baada ya wengi wa Wanafunzi hao ambao wengi wao kuishi maisha magumu kutokana na kuishiwa pesa za chakula naa nyingine za matumizi ya kawaida ya kila siku ambayo walikuwa wanategemea pesa kutoka kwa bodi ya mikopo maana wengi wametokea familia zenye hali mbaya kiuchumi. 

Tunajitahidi kupata uongozi wa Chuo na serikali ya wanafunzi ili kujua msimamo wao na hatima yya mgomo huo.
BADO HAKIJAELEWEKA UDSM, WANAFUNZI WAGOMA KUINGIA MADARASANI WATAKA WAINGIZIWE PESA ZA BOOM BADO HAKIJAELEWEKA UDSM, WANAFUNZI WAGOMA KUINGIA MADARASANI WATAKA WAINGIZIWE PESA ZA BOOM Reviewed by WANGOFIRA on 02:10:00 Rating: 5
Powered by Blogger.