ABDULLAH AMWACHIA ULAJI HAMAD RASHID



Mwenyekiti wa  Chama cha ADC ,Hamad Rashid.
Mwenyekiti wa  Chama cha ADC ,Hamad Rashid. 

Dar e s Salaam. Kuondoka madarakani kwa Mwenyekiti wa  Chama cha ADC, Said Miraji Abdullah, kumetoa nafasi kwa Hamad Rashid kurithi kiti chake.
Miraji  ameondoka kutokana na kutofautiana na viongozi kuhusu uamuzi wa chama hicho kushiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliofanyika Machi 20, mwaka huu.
Chama  hicho pia kimemchagua Doyo Hassan Doyo kuwa Katibu Mkuu aliyechukua nafasi ya Lydia Bendera ambaye alikuwa akimuunga mkono Abdullah kwa kutotaka chama hicho kisishiriki uchaguzi huo.
Akizungumzia hatua hiyo, makamu mwenyekiti wa ADC, Adelastella Mkilindi amesema chama hicho kimefikia uamuzi huo ili kutimiza matakwa ya kikatiba yanayotaka kuwa na uongozi kamili.

ABDULLAH AMWACHIA ULAJI HAMAD RASHID ABDULLAH AMWACHIA ULAJI HAMAD RASHID Reviewed by WANGOFIRA on 20:06:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.