14 Wakamatwa Kwa Tuhuma ya Ujambazi,Yumo Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwika

Polisi imewakamata watuhumiwa 14 wa ujambazi na unyang'anyi wa kutumia silaha, akiwemo Kelvine Shao, mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya kutwa ya Mwika mkoani Kilimanjaro. 
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro kamishna msaidizi(ACP) Wilboroad Mtufungwa amedhibitrisha kukamatwa kwa watu hao ambao kati yao yumo pia mwanamke kikongwe Upendo Rajabu mganga wa kienyeji.

Amesema katika msako huo pia wamefanikiwa kukamata bunduki aina ya Shortgun na risasi tatu zikiwa zimefunikwa chini ya gari moja aina ya Toyota Noah pikipiki tatu pamoja na mapanga.

Aidha amesema pamoja na jeshi hilo kutoa elimu mashuleni kuhusu masuala ya uhalifu lakini bado kumekuwapo na wimbi kubwa la vijana wanao jihusisha na matukio ya ujambazi.

Katika kipindi kisichozidi miezi minne wafanyabiashara watano wameuwa kwa kupigwa risasi na kisha wauaji kutokomea pasipojulikana.
 
                                     Chanzo-ITV
14 Wakamatwa Kwa Tuhuma ya Ujambazi,Yumo Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwika 14 Wakamatwa Kwa Tuhuma ya Ujambazi,Yumo Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwika Reviewed by Unknown on 20:29:00 Rating: 5
Powered by Blogger.