WARAKA WA WAZIRI WA AFYA UDSM KWA WAUGUZI WA MUHIMBILI(MNH).


Katika muda wangu wote wa kuwatumikia wana DARUSO toka mwaka Jana nimepata kuhusika moja kwa moja na matatizo ya Afya ya wanafunzi wengi katika hospitali mbalimbali Kama vile Muhimbili, Kairuki na Mwananyamala

Mengi nimeona na kujifunza katika huduma hiyo Muhimu kwa jamii

Wapo madaktari na wauguzi wanaojituma sana na Mungu awabariki. Lakini jicho langu limeona wauguzi na madakatari wakali na wenye kauli chafu kwa wagonjwa (Mungu awasamehe) mambo haya ninayotaka niseme leo yananikumbusha jinsi mwanafunzi mwenzetu Michael Ogendo alivofariki kwa uzembe wa wauguzi katika hosipitali ya Muhimbili wodi ya MWAISELA kwa kugoma makusudi kumwongezea damu mgonjwa kwa kudai kuwa damu hakuna lakini hata ndugu zake walipojitolea Damu bado hawakumwekea jambo lililosababisha Kifo chake (R.I.P OGENDO MUNGU WASAMEHE WAUGUZI HAO)


 Leo tena Mwanafunzi mwenzetu KAWANARA LONA JOSHUA college ya UDBS amekumbwa na mkasa wa hizi konakona

Joshua amepatwa na tatizo la kupalalaizi kabla ya Pasaka hivo kupelekea kulazwa katika hospitali hii ya Muhimbili (Mungu ni mwema anaendelea vizuri)

Sasa cha ajabu Chief Phamacisit wa Muhimbili Bwana BUMA na wenzake ambae kwa sasa namtambua Kama JIPU lilioiva alipindisha uhalali wa Joshua kupata huduma kwa Utaratibu wa bima- NHIF na kupelekea Mgonjwa huyu kijana anaejihudumia kwa pesa zake za kusaka na jasho huku akiwaza Ada lakini huku sehemu nyingine akiisaidia familia yao ya hali ya chini Kugharamia mpaka Jana kiasi cha Milioni moja na laki nane (1.8mil)

Jambo hili la kuumiza Sana liliigusa Ofisi ya Mshauri wa Wanafunzi -Kitengo cha Afya( ambayo binafsi nakili imekuwa msaada mkubwa sana kwa Serikali ya DARUSO na Wana DARUSO)

Jambo hili kwa kushirikiana na Kijana Mahili mwana CoET ndg Kelvin (MUNGU ambariki Sana) anaemuuguza Mgonjwa jana tar 5/4/2016 ulifanyika utaribu wa kumwona Mkurugenzi wa tiba Muhimbili Dr. Swai ambae aliita kikao haraka na Chief pharmacist ndg Buma na wenzake na kulibaini tatizo huku utaratibu wa kurejeshewa pesa yote mil 1.8 ukikamilika leo

Huyu mama Anastahili pongezi na hawa ndo viongozi Tunaowataka

Ombi langu Madaktari na wahudumu mlio na tabia hizi tambueni mmepewa dhamana kubwa kwanza na Mungu lakini Pili na Serikali kuwahudumia wananchi wote wenye hali zote

Mimi Kama Kiongozi sioni uhalali na kuendelea na wahudumu wasio jali utu hali za watu waliopewa dhamana ya kuwahudumia hivo nashauri ngazi za juu kutupa jicho la tatu kwa watu hawa.

Gregory paul
N.Waziri Afya na Chakula DARUSO UDSM
0657 221113
WARAKA WA WAZIRI WA AFYA UDSM KWA WAUGUZI WA MUHIMBILI(MNH). WARAKA WA WAZIRI WA AFYA UDSM KWA WAUGUZI WA MUHIMBILI(MNH). Reviewed by WANGOFIRA on 01:37:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.