WARAKA KWA WANAZUONI NCHINI.
Na
SHITINDI VENANCE.
KATIKA MAISHA YA CHUO.
Katika
maisha haya wengi wanaishi maisha ya starehe na hii ni mahususi kwa watu wenye
mkopo (boom), Lakini cha ajabu kundi hilihili hugeuka ghafla kama kinyonga na
kuishi maisha magumu wakati pesa za boom zikiisha. Kinapofika kipindi cha mwisho wa muda wa boom
hilo na bahati mbaya zaidi kama boom linalofwata litacheleweshwa na bodi basi
hali huwa mbaya zaidi kufikia watu kukomnika na wengine kupiga shato pori.
MAISHA
BAADA YA CHUO.
Wengi wanapojiunga na chuo kwa mara ya kwanza na
kubahatika kupewa mkopo kutoka bodi ya mikopo, hujisahau na kuamini kuwa maisha
ya kupewa mkopo ni ya milele na kamwe hayatakoma na hivyo kutumia pesa
wanavyoona inawafaa. Lakini mwisho wa siku ujikuta wakiwa katika wakati mgumu
na kuanza kuombaomba.
Waswahili husema hakuna marefu yasiyo na ncha,
hufika pasipo hodi, ambayo nami nakubaliana nayo pasipo hata shaka. Hivyo ni
wakati muafaka kwa wanazuoni kutengeneza nidhamu ya matumizi ya pesa wawapo
chuoni maana maisha hubadilika ghafla.
Katika maisha mpya baada ya chuo huko
mwanazuoni hujikuta hamiliki kitu chochote zaidi ya kompyuta pakata (PC) na radio
maarufu kama sabufa.
Hapa hugutuka kuwa hana chumba cha kulala wala kodi ya kupanga, hana mtaji wa kuanza biashara wala biashara inayoishi, kifupi hana mbele wala nyuma, na matokeo yake atarudi nyumbani kwa baba na mama kuendeleza unyonyaji na utegemezi kwa wazazi aliowanyonya takribani miongo zaidi ya miwili ya maisha yake.
Swala
hili linamadhala makubwa yasiyoonekana moja kwa moja kwa muhusika na jamii kwa
ujumla, hii ni kwasababu
Kwanza mtu huyu atawakatisha tamaa wadogozake wengine na hata wanajamii
kuwekeza katika ELIMU wakilejelea maisha magumu aishiyo mwanazuoni huyu, maisha
ya utegemezi usiokoma ikilinganishwa na wale wasio na elimu kubwa.
Pili
kulalama hovyohovyo kwa kukosa ajira kwa msomi huyu kutajenga picha mbaya kwa
wanajamii kwamba ukisoma lazima uajiliwe na kama hutoajiliwa basi mambo
yatakuwia vigumu na wengi wa wanajamii watajengeka katika mtazamo huo hasi
katika karne ya 21.
Tatu
mwanazuoni husika ataishusha hadhi ya mwanazuoni kutoka kuwa mtatuzi wa
matatizo (problem solver) na kuwa muelezea matatizo kitu ambacho si dira ya
elimu popote duniani.
WITO WANGU KWA WANAZUONI WENZANGU.
Wanazuoni wote wakike kwa wakiume wanapaswa kutambua kuwa ndio taifa la Leo, na kila kifanyikacho kina matokeo kwa jamii ambayo yawezakuwa hasi au chanya hivyo kuanzia sasa inapaswa kufanya mambo yafananayo na hadhi ya wanazuoni.
Pia
inapaswa kujua fika kuwa pesa zitolewazo zinatosha, ikiwa mtu kujibana na
kuanzisha miradi inayoweza kujiendesha yenyewe pasipo na usimamizi mkubwa
kutoka kwa mhusika. na hivyo kujiingizia kipato katika maisha ya chuo na hata
maisha baada ya chuo. Na kurudisha heshima ya mwanazuoni na hata kuliingizia
taifa letu Mapato kupitia kodi.
Mwisho
kuzaliwa masikini si kosa kosa ni kufa masikini, Mungu wabarikini sana
mnapofanya maamuzi ya matumizi mazuri ya pesa za boom.
Waraka
huu umeandikwa na shitindi Venance, waziri wa mikopo Udsm, waweza wasiliana kwa
namba 0759704444 au 0676705440.
WARAKA KWA WANAZUONI NCHINI.
Reviewed by WANGOFIRA
on
20:48:00
Rating:
No comments: