VIJIJI ZAIDI YA 5000 NJOMBE KUNUFAIKA NA UMEME WA REA

Jumla ya wateja 5,235 kutoka vijiji 78 vya Mkoa wa Njombe wanatarajiwa kunufaika na huduma ya umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili, ambayo itakamilika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Mmoja wa wananchi katika kijiji cha Isindagosi – Njombe, akitoa maoni yake kuhusu utekelezwaji wa miradi ya umeme vijijini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara mkoani humo hivi karibuni kutembelea miradi ya umeme vijijini.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anatory Choya aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa mkoani humo.
Akitoa mchanganuo wa idadi ya vijiji vitakavyonufaika na mradi husika kutoka kila Wilaya ya Mkoa huo, Choya alisema kuwa Wilaya ya Njombe ni vijiji 31, Makambako vijiji 20, Makete vijiji 21 na Ludewa vijiji sita.
Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Njia ya Umeme wa Msongo wa Kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea, Mhandisi Didas Lyamuya, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakati Wajumbe wa Kamati hiyo walipokuwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, kabla ya kutembelea miradi ya umeme vijijini inayotekelezwa mkoani humo.

Aidha, Kaimu Mkuu wa Mkoa, aliwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge kuwa, Mkoa wa Njombe una miradi mingine 18 ya uzalishaji wa umeme ambayo iko katika hatua mbalimbali za ujenzi na kwamba miradi hiyo inafadhiliwa na sekta binafsi, mashirika ya dini pamoja na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Naye Meneja wa TANESCO Mkoa wa Njombe, Mhandisi Emmanuel Kachewa, akielezea zaidi kuhusu utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili mkoani Njombe, alisema kuwa ujenzi wa laini kubwa, ufungaji wa mashine umba (transfoma), ujenzi wa njia ndogo na usambazaji wa umeme kwa wateja ulianza rasmi mwezi Oktoba 2013 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni 30 mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (wa pili kutoka kulia) akijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anatory Choya (kulia), wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini (hawapo pichani), mkoani humo hivi karibuni, kukagua utekelezwaji wa miradi ya umeme vijijini. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje.

Aidha, Mhandisi Kachewa alieleza kuwa, gharama ya mradi kwa eneo la Mkoa wa Njombe ni shilingi bilioni 24 za Tanzania na kwamba mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi Lucky Exports kutoka nchini India.
Kwa upande wake, Meneja anayesimamia mradi wa ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea, Mhandisi Didas Lyamuya aliiambia Kamati hiyo ya Bunge kuwa mradi huo ni moja kati ya miradi ya mifumo ya kusafirisha na kusambaza umeme unaotekelezwa katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Njombe, Mhandisi Emmanuel Kachewa (mwenye suti ya bluu-kushoto), akiwapa maelezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kuhusu sehemu ya kuchukulia umeme (taping point) iliyopo kijiji cha Italahumba – Njombe, wakati wa ziara ya Kamati hiyo kukagua miradi ya umeme vijijini mkoani humo hivi karibuni.

Mhandisi Lyamuya alisema kuwa, lengo la mradi husika ni kupeleka na kuboresha umeme katika maeneo ya uzalishaji na majumbani katika vijiji na miji iliyopo katika mikoa ya Njombe na Ruvuma hususan wilaya ya Njombe, Ludewa, Songea mjini, Songea vijijini, Namtumbo na Mbinga.
Akielezea kuhusu gharama za mradi, alisema kuwa kwa upande wa Mkandarasi wa usambazaji kutoka kampuni ya ISOLUX ni shilingi bilioni 73, Mkandarasi wa mfumo wa usafirishaji umeme ambaye ni Kampuni ya Kalpataru shilingi bilioni 65, Mkandarasi wa vituo vya kupooza umeme, Kampuni ya JV Shandong Taikai-Norinco, shilingi bilioni 26 na Mhandisi mshauri, Kampuni ya SWECO shilingi bilioni 15.
Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini mkoani Njombe, ni mwendelezo wa ziara ambazo Kamati hiyo inafanya sehemu mbalimbali nchini, kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa chini ya Wizara ya Nishati na Madini.
Imeandaliwa na:
Veronica Simba,
Afisa Habari,
Wizara ya Nishati na Madini,
VIJIJI ZAIDI YA 5000 NJOMBE KUNUFAIKA NA UMEME WA REA VIJIJI ZAIDI YA 5000 NJOMBE KUNUFAIKA NA UMEME WA REA Reviewed by WANGOFIRA on 11:53:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.