Vigogo wa TRA ,Harry Kitillya na Wenzake Wawili Warudishwa Tena Rumande Hadi Tarehe 3 Mwezi Ujao

 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imesita kutoa uamuzi wa kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni kwa madai, jalada lake limeitishwa Mahakama Kuu. 

Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwezekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic. 

Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu amesema kuwa, hana mamlaka ya kutolea uamuzi wa kesi hiyo kutokana na jarada lake kuitishwa Mahakama Kuu leo asubuhi. 

Kutokana na hali hiyo Hakimu Mchaura amesema kwamba, kesi itatajwa tena tarehe 12 Mei mwaka huu na watuhumiwa watarudishwa rumande. 

Muda mfupi baada ya hakimu Mchaura kusema hivyo, Kitilya na wenzake walirudishwa tena mbele ya Hakimu huyo baada ya hakimu kupata amri kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akimtaka kesi hiyo itajwe Mei 3, mwaka huu badala ya tarehe 12 Mei mwaka huu aliyoipanga awali. 

Hakimu Mchauru amesema, sababu za kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi itatajwa tena tarehe 3 Mei mwaka huu na yale yaliyozungumzwa asubuhi yatabaki kama ilivyo.
Vigogo wa TRA ,Harry Kitillya na Wenzake Wawili Warudishwa Tena Rumande Hadi Tarehe 3 Mwezi Ujao Vigogo wa TRA ,Harry Kitillya na Wenzake Wawili Warudishwa Tena Rumande Hadi Tarehe 3 Mwezi Ujao Reviewed by WANGOFIRA on 23:15:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.