NI MTAZAMO TU, KUHUSU DARUSO IJAYO

NA, 
Manoah Kefa William Mwakalesi.

Kwa muda mrefu sasa tumeshuhudia siasa na kampeni za kipekee na zisizo na mvuto tarajali UDSM, huku wanazuoni wengi kutia ndani mimi mwenyewe tukionesha wazi kukerwa na ujuha uliofanywa na tume ya uchaguzi kwa kuleta wagombea ambao huenda walionesha mtazamo wa kikada na kushindwa kusababisha kampeni kuwa na mvuto. Lengo kuu ni kupata watu watakaoweza kuyasemea matatizo ya wanaUDSM kwa Uhuru na kutohofu mabwenyenye waliowatuma. Tamaa yetu ni kuona viongoU watakaoteuliwa wanasimamia maslahi ya umma na kujisimamia katika kutekeleza ilani zao na kuwatetea wanaUDSM.

Lakini ni wazi kuwa bado DARUSO itapata Rais ambaye atashikilia maslahi mpana ya wanafunzi na atapaswa kuyatetea popote. Ikiwa tutakuwa na mbovu zaidi ndivyo mambo yatakavyoenda mrama na kuua serikali ya wanafunzi. Kwa mantiki hiyo, kuna kila sababu, Pasi na kificho kutafuta angalau mmoja anyeweza kuwa KIONGOZI na sio mfano wa kiongozi katika serikali ijayo. Kiongozi huyu atapaswa kuweka mahitaji ya wanafunzi Mbele, asahau chama kilichomsukuma kwa namna yoyote, ajiepushe na chama ili afanikiwe, ajitathmini maana ya kuwatumikia wanaudsm na sio chama.

Kuna mambo machache nionayo yanafaa kuniongoza ili mtu huyu aweze kuwatumikia wanadaruso.

1. Aweze kuwasemea na kujisemea yeye mwenyewe na kuwa na msimamo wake. Kwa uzoefu wangu katika Uongozi, Rais wa DARUSO na makam wanapaswa kuwa na uwezo usio na shaka wa kujenga, kutetea na kuisimamia hoja. Hii ndio silaha juu ya Rais wa DARUSO na makamu  Kwani bila kuweza kusimama na kutetea lile aaminilo, atakuwa bubu au bwege katika vikao vya maamuzi ya juu ya chuo. Hakuna ajuaye mambo yanvyokuwa katika Senate, council, SAC, DSCC,  na vikao vingi vya chuo na hakuna mrejesho wowote  ambao wanafunzi hupata. Ni vema pasipo na kijicho, tujiridhishe na uwezo wa Ndugu huyu.
Kuna mambo machache nionayo yanafaa kuniongoza ili mtu huyu aweze kuwatumikia wanadaruso.

2. Makini na mwenye ubunifu. Ni vema Rais awe na mikakati yake mwenyewe ya kibunifu kadiri serikali iwapo kazini. Awe na akili pana na kuweza kujua mengi yanayoweza kufanywa, na sio kuletewa hoja kila Leo na viongozi wengine huku yeye akijistarehesha.

3. Awe na uwezo wa kudhibiti serikali, aiongoze, awe mkuu wa serikali kwa Maneno na matendo. Hapa naona ipo haja ya Rais kuwa na sauti ya kuongoza, yaani kuwaunganisha anawaongoza katika moyo mmoja, waone wao ni subordinates na hiyo iwe ndani yao. Awakusanye na kujenga umoja kwa hekima lakini akiwa na uimara mkubwa.

4. Usikivu na kukubali ushauri. DARUSO nyingi huharibika kwa sababu ya jeuri za marais na kiburi kuelekea baraza la mawaziri, vice President na wanadaruso,  hivyo ni lazima sifa hizo ziwe zake na adhihirishe tangu awali.
Ningeweza kusema mengi, ni kweli Sera nyingi zinazoahidiwa na wagombea ni kazi kutekelezeka na ni Nadra huku nyingine xikiwa hekaya za uswahilini, lakini uwezo wa kuzitetea licha ya ubovu wazo hutusaidia kujua kina cha mawazo ys hekima kwa wagombea hawa.

Ikiwa ukiwachunguza vema, pasipo na upendeleo, ERASMI LEONE aneonesha uwezo wa kadiri. Wacha tuweke pembeni makando kando yanayowahusu wagombea wote, kwa Kuwa ni wazi wote ni watoto wa baba mmoja, huku mmoja akikamatwa na majibu siku ya screening, Erasmi Leone ameonesha uwezo wa kujenga hoja, kutetea na angalau kuonesha kuwa, ikiwa atajitenga na wahafidhina katika uteuzi wa baraza lake la mawaziri, ikiwa atajitenga na wenye pupa ya sifa kuwa wao ndio wamemweka madarakani, na ikiwa atasimama kidete kutetea umma wa wanafunzi, basi ataweza kusukuma gurudumu Mbele pasi na hofu wala mawaa.

Ni vema tukakumbuka kuwa chuo kikuu cha DSM kina colleges 7, schools 4 na institutes 2 ambazo ni member wa DARUSO na kuna undergraduate students. Hivyo, ni wazi kuwa kila college inauwezo wa kutoa Rais ambaye atakuwa na uwezo wa kushawishi na kuonesha uwezo wa kuongoza chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Ni vema kutafakari mustakabali wa DARUSO na kuona umuhimu wayo katika kutetea wanafunzi.

Ashanteni



NI MTAZAMO TU, KUHUSU DARUSO IJAYO NI MTAZAMO TU, KUHUSU DARUSO IJAYO Reviewed by WANGOFIRA on 19:43:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.