MTOTO WA KITANZANIA ATOA AHUTUBIA VIONGOZI MBALIMBALI WA DUNIA KWENYE MKUTANO WA UN.

Mtoto Mtanzania mwenye umri wa miaka 16 Getrude Clement kutokea Mwanza amehutubia mbele ya viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa umoja wa mataifa akiwa mwenye kujiamini na kutoonekana kuwa na hofu japo anaongea kwenye jukwaa ambalo linatazamwa na viongozi mbalimbali.
Mataifa zaidi ya 150 yalitia saini makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Marekani ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon ndio alimkaribisha Getrude kuongea kwa kusema ‘ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana
Getrude alianza kwa kuwasalimia waalikwa huku ikiripotiwa Maraisi 60 walihudhuria na kisha akaeleza kuwawakilisha vijana na watoto ambapo alizungumzia mabadiliko ya tabia nchi, hatari yake na kwamba wamekua wakifikisha ujumbe kwa Wananchi juu ya mabadiliko hayo kama anavyoonekana kwenye hii video hapa chini.
Getrude
MTOTO WA KITANZANIA ATOA AHUTUBIA VIONGOZI MBALIMBALI WA DUNIA KWENYE MKUTANO WA UN. MTOTO WA KITANZANIA ATOA AHUTUBIA VIONGOZI MBALIMBALI WA DUNIA KWENYE MKUTANO WA UN. Reviewed by WANGOFIRA on 22:15:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.