MAMBO TAYARI, HATMA YA DARUSO 2016/2017 MIKONONI MWA HAWA....

Image result for daruso udsm
WAJUMBE WA TUME YA RUFAA YA UCHAGUZI WA DARUSO 2016/2017.
Kama walivyochaguliwa na kikao cha mwisho cha bunge la Daruso jana 09/04/2016.
1. Alpha Abdallah (SJMC)
2. Kiyagi Steven  (SoED)
3. Shitindi Venance (CoSS)
4. Ibrahim Shija (CoHU)
5. Kimario Seraphin (CoICT)
6. Embas Julius  (CoNAS)
7. Asimwa Owakisha (IKS)
8. Alexander Mapunda (CoET)
9. Elihuruma Nyari (UDBS)
10. Frank Katyega (UDSoL).

Wajumbe hawa ndiyo watakaokutana kesho Jumatatu saa nne kamili asubuhi kwaajili ya kufanya uchaguzi wa mwenyekiti na Katibu wa tume ya rufaa ya uchaguzi.

Uchaguzi wa mwenyekiti na Katibu wa tume hiyo unatarajia kuwa chini ya usimamizi wa Ofisi ya Spika wa bunge la Daruso na Ofisi ya Mshauri wa wanafunzi (Dean of students).
Majukumu makubwa ya tume ya rufaa ya Uchaguzi wa Daruso ni kupokea rufaa zinazotokana na maamuzi ya tume ya uchaguzi ya Daruso.

Kikatiba chombo hiki ndicho chenye maamuzi ya mwisho juu ya mchakato wa uchaguzi wa Daruso hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni Tume ya rufaa ya uchaguzi imekuwa dhaifu, isiyo na meno na isiyo na muda wa kutosha wa kushughulikia malalamiko yanayopelekwa katika tume hiyo kutokana na ratiba ya uchaguzi kuibana Tume hiyo na mara nyingine ikishughulikia malalamiko ilihali tayari uchaguzi umeingia katika hatua zingine.
MAMBO TAYARI, HATMA YA DARUSO 2016/2017 MIKONONI MWA HAWA.... MAMBO TAYARI, HATMA YA DARUSO 2016/2017 MIKONONI MWA HAWA.... Reviewed by WANGOFIRA on 13:12:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.