MADEREVA WA MALORI MAKUBWA WAKAIDI AGIZO LA SERIKALI.

 
Siku chache baada ya Serikali kuzindua daraja jipya la Kigamboni jiji Dar es Salaam na kukataza Magari yenye uzito zaidi ya tani kumi kutopita katika daraja hilo baadhi ya madereva wasiofuata sheria wamekuwa wakikiuka agizo hilo na kuonekana kupita katika daraja hilo.
 

Akitekeleza majukumu yake Inspekta Hassan Amadi ambaye ni mkuu wa usalama barabani wilaya kipolisi Kigamboni amesema kwamba ifike kipindi madereva waache kuvunja sheria na kufuata maelekezo nakuwataka madereva wengine wanaovunja sheria sehemu mbali mbali hususani wanao tumia daraja hilo kufuata sheria zilizowekwa na kuepuka makosa kama hayo.


 

Naye dereva aliyevunja sharia akijaribu kujitetea amesema kwamba hkufahamu utaratibu mzima wa upitaji katika barabara hiyo hivyo anakiri kosa alilofanya nakuwasihi madereva wenzake wafuate sheria Barabarani.
MADEREVA WA MALORI MAKUBWA WAKAIDI AGIZO LA SERIKALI. MADEREVA WA MALORI MAKUBWA WAKAIDI AGIZO LA SERIKALI. Reviewed by WANGOFIRA on 21:22:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.