KUELEKEA DARUSO MPYA

Kwa muda huu ambao tume imekwishatoa ratiba kamili ya mustakabali wa DARUSO hasa katika uchaguzi unaoelekea kufanyika katika siku za usoni, nami ningependa kushare  nanyi mambo machache hasa ukizingatia yale yote yaliyowahi jadiliwa na pengine yanayozidi jadiliwa kuhusu hasa uamuzi wangu binafsi katika nafasi nitakayogombea katika uchaguzi huu, na haya ndiyo maamuzi niliyoyafikia baada ya kupokea ushauri kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zangu, viongozi wa Daruso na wanaharakati wa siasa ya Daruso pamoja na wanaDaruso baadhi.

Itakumbukwa kwamba kiongozi yeyote ili awe makini lazima awe amejipanga na kujidhatiti katika kuchukua nafasi yoyote ile ambayo yeye binafsi anaona inamtosha na kwamba anaona ataitendea haki, "the issue is not the position but the IMPACTS", Kuelekea uchaguzi huu nimejikuta nina changamoto kubwa hasa ukizingatia kwamba kulikuwa na sehemu mbili zinazovutana, sehemu ya kwanza ikinihitaji kugombea urais na sehemu ya pili ikinihitaji kugombea sehemu ambayo nawiwa kugombea (>>>) ambayo ni kuliongoza bunge la DARUSO.

Baada ya kulitambua hilo na baada ya kutambua nia ya dhati ya kila upande niliamua kusikiliza na hata kuwaomba ushauri wa mawazo wadau mbalimbali ambapo kwa namna ya pekee nipende kuwashukuru kwa utayari wao wa kunishauri maana kwenye maisha "you will never walk alone" nami sitaweza kusimama na wala kutembea peke yangu bila wao, maana mimi bila wao bado sijakamilika!

Ndugu zangu wengi wanaweza fikiria kwamba labda nimewaangusha kwa kuamua maamuzi ambayo nayachukua la hasha!! nawashukuru kwakuwa katika watu mliowafikiria kugombea urais nami nilikuwa miongoni mwao naamini hamkunifikiria kwa kwasababu mnanifahamu bali mlinifikiria kwasababu ya uwezo ambao mliamini kwa dhati kabisa kwamba ninao na katika hilo naweza sema AKSANTENI SANA!

Toka siku ya kwanza nafika chuoni nilihitaji kuijua zaidi DARUSO na pengine kuwa sehemu kubwa ya kuishauri na kuhakikisha kwamba tunaDARUSO YENYE TIJA, kama ile ambayo ilijengwa na baadhi ya watu katika kipindi kilichopita, ndoto hiyo bado ninayo lakini si kweli kwamba nitatimiza ndoto hiyo kwa kuwa RAIS WA DARUSO, nafasi ambayo mimi naiona ina mambo mengi na inahitaji mtu awe amejipanga kuchukua majukumu yake na si tu mtu kuitwa RAIS lakini hauishi URAIS wake!

Naamua mara baada ya kuwasikiliza wanaDARUSO kwenda kugombea nafasi ambayo naamini nikipewa baraka na kuaminiwa nitahakikisha kupitia huko naijenga DARUSO YENYE TIJA na si BORA DARUSO! sehemu ambayo naamini nitatekeleza majukumu yangu with passion kwa kuwa nilijiandaa na ninamaono ya kuyatimiza na si sehemu ambayo sikujiandaa ingawaje baadhi ya wanaDARUSO wanaona itanifaa.

Nawaomba sasa wale ndugu zangu wote ambao kwa nia njema walinishauri kugombea URAIS waungane nami katika nia yangu hii na maamuzi yangu haya ya kutogombea hapo bali kugombea sehemu ambayo naamini nitaitendea haki na HII ISICHUKULIWE KAMA KAMPENI NA NDIYO MAANA SIWEKI VIPAOMBELE HUMU, na waniunge mkono katika maamuzi hayo na hata muda ukifika wawe tayari kuniunga mkono na wasijisikie kusalitiwa na maamuzi yangu kwasababu wote tuna lengo moja la kuijenga DARUSO IMARA NA YENYE TIJA!

Rai yangu kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya DARUSO ni kwamba, tusigombee nafasi ili tu, tuwe viongozi na pengine kuziwaza CV bali tugombee uongozi kwa nia thabiti ya kutaka kuijenga DARUSO na kuwatumikia wanaDARUSO wote waliotuamini kwa ujumla wao na si kwa malengo ya kujinufaisha tukumbuke, UONGOZI NI DHAMANA!

AKSANTENI SANA!!


MWAMPAGHALE, ANDREW A. (LL.B.-UDSM)
KUELEKEA DARUSO MPYA KUELEKEA DARUSO MPYA Reviewed by WANGOFIRA on 21:02:00 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.